Friday, September 21, 2012

MHARIRI AMZIMIKIA KIMOBITEL

Mhariri wa gazeti moja maarufu hapa nchini anayeandika habari muhimu zinazowahusu watawala wa nchi mbali mbali Duniani Mr. Mussa akishoo luv na mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bendi anayepiga mzigo ndani ya Extra Bongo, Khadija Mnoga aka Kimobitel walipokutana maeneo ya KAPINGAZ Pub maeneo ya Kinondoni.
Kimobitel akisimulia jambo mbele ya wapenzi na wadau mbali mbali wa muziki wa dansi.
Mudi Trafiki akifuatilia kwa umakini moja ya mechi zilizojiri jioni ya jana, pale Simba waliojizolea pointi muhimu na Yanga kopoteza,
Mwandishi mkongwe wa habari za michezo na burudani wa magazeti ya kampuni fulani ambayo maskani yake ypo Kinondoni akifurahia jambo na mmoja wapenzi wa magazeti ya Burudani na michezo.
Mhariri Mussa hapa akiuliza wadau, namnukuu "Juu ya nini mimi kumpa Shavu KIMOBITEL ntahakikisha namsapoti kwenye kazi zake mpaka dunia imtambue" mwisho wa kunukuu.
Hapa Kimobitel akifurahia jambo na meneja wa Extra bongo Mujibu wa Majibu walipokutana maeneo ya Kinondoni ndani ya KAPINGAZ PUB.

No comments:

Post a Comment