Friday, September 21, 2012

WAJUMBE WA CHADEMA WAKATAA KUPOKEA BARABARA ILIYOJENGWA NA MGODI.

Tarime.


WAJUMBE wa Serikali ya kijiji cha Nyamwaga Wilayani Tarime Mkoani Mara kupitia chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA  wamekataa kupokea  mradi wa ujenzi wa barabara ya kilomita mbili inayopita ndani ya kijiji hicho  iliyojengwa na Mgodi wa dhahabu wa Africa Barrick Gold Mine(ABG)  kwa madai kuwa  barabara imejengwa  kwa kiwango cha chini kisichostaili na wala haikubainishwa kiasi cha pesa kilichotumika kujenga barabra.



Hayo yalibainika juzi  wakati mgodi wa ABG ukikabidhi barabara  ya kilomita 2 katika  uongozi wa Serikali ya kijiji cha Nyamwaga iliyojengwa na Mgodi iliyokabidhiwa na Kaimu meneja  wa Mgodi Mark Luyt



Wajumbe walisema kuwa hata kama mgodi umetoa msaada wa ujenzi ulipaswa  kubainisha  km za  barabara na kiasi cha pesa kilichotumika kujenga barabara pamoja hivyo kudai kuwa barabara hiyo imepokelewa na  Mwenyekiti wa jijiji na Diwani ambao ni  viongozi wa CCM na siyo Chadema kwa madai kuwa barabara  imejengwa  chini ya kiwango na haina makaravati.


 “Meneja  jua kuwa hii barabara umekabidhi kwa Mwenyekiti na Diwani nasiyo Serikali ya kijiji sisi kama wajumbe wa Chadema  hatujaipokea huwezi kukabidhi barabara bila kutueleza imejengwa kwa pesa ngapi na ni kilomita ngapi,barabara imelipuliwa haina hata makaravati! Msidhani sisi ni watoto wadogo tuna akili timamu hata kama ni msaada   kwakuwa hamjasema imejengwa kwa pesa ngapi sisi wajumbe hatujaipokea”alisema Chacha Mwita



Mabali na wajumbe hao wa Chadema  pia baadhi ya wananchi waliokuwepo wakati wa makabidhiano ya barabara waliulalamikia mgodi na Serikali ya kijiji kwa kufanya makabidhiano pasipo kuwashirikisha wananchi wa jijiji hicho ili nao wapate fursa ya kutoa hoja zao na kuuliza maswali kuhusiana na ujenzi wa barabara.



“Serikali inafanyanje mambo mbila kushirikisha wananchi wake? Kwanini hawakualika wananchi kwenye hayo makabidhiano wanakabidhiwa  tu viongozi wa Serikali ya kijiji! cha kushangaza Meneja kakibidhi barabara bila kutuambia imejengwa  kwa pesa ngapi na nikwanini wakabidhi barabara ya km 2 na wakait Serikali ya kijiji ilituambia  kwa awamu ya kwanza watajenga barabara ya kilo km5 baadaye watamalizia km zingine 5 matokeo yake wanakabidhi km2 zilizobaki zitajengwa na nani na lini? Na histoshe wakafyeka miti wakafukia visima vya watu bila hata fidia yoyote”alisema Sabyo Maricha.


Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamwaga Sasi Kirigiti alisema hawakuweza kualika wananchi kwakuwa mgodi ulichelewa kuwapatia taarifa ambayo ilitolewa siku moja kabla ya kufanyika kwa makabidhiano na kwamba kuwa  barabara hiyo ya km 2 imejengwa kwa sh milioni 70 na kwamba barabara hiyo imejengwa kwa msaada wa mgodi kwani haikuwa kwenye mkataba.


Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo  iliyoko ndani ya kijiji cha Nyamwaga Chacha Msabi alisema barabara imejengwa  kulingana na kiasi cha pesa kilichotolewa na mgodi wa ABG na kwamba  amejenga barabara nyenye urefu wa km 2 ambayo gharama yake ni Dora 80 za kimalekani hivyo kulingana na pesa kidogo haikutosha kuweka makaravati



Kaimu Meneja wa mgodi wa ABG Mark Luyt alisema km  35 za uferu wa barabara  zimejengwa na mgodi  ndani ya vijiji vinavyozunguka mgodi ambapo sh milioni 254, 55,5 500 sawa na dola laki moja na 65 elfu ambapo midadi mingine itanjengwa kwa awamu tofauti tofauti japo hakubainisha kiwango halisi katika ujenzi wa barabara ya Nyamwaga.


No comments:

Post a Comment