Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limempongeza kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Ally Augustino umri wa Miaka (20) baada ya kufanya kitendo cha kijasiri kwa kudandia gari lililosababisha ajali na kukimbia, kisha kufanya mawasiliano na askari Polisi mkoani humo na kufanikisha kukamatwa kwa gari hiyo.
Akizungumzia Tukio hilo Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamisha Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw.
ZELOTHE STEPEN alisema lilitokea majira ya saa mbili usiku jana katika kijiji
cha Chilonwa Wilayani Chamwino na kusababisha kifo kwa mtembea kwa miguu
aliyejulikana kwa jina Daniel Chilomboli, mgogo mwenye umri wa miaka (30)
“ Gari lilipomgonga mtembea
kwa miguu huyo lilipunguza kasi kidogo na
kusimama lakini kwa kuwa watu walikuwa wakipiga mayowe na kukusanyika kwa wingi
Dereva aliwasha gari na kuanza kuondoka ndipo Kijana huyo bila kuchelewa
akalidandia kwa nyuma na kuanza kufanya mawasiliano na Askari kwa kutumia simu”
alielezea Bw. Zelothe Stephen
Alilitaja gari
lilosababisha ajali hiyo ya kumgonga mtembea kwa miguu kuwa ni lenye usajili wa namba T.775 ATD MITSUBISHI CANTER ambalo ubavuni lilonyesha
kumilikiwa na Bw. NJIUKA E.R.M WA SANDUKU LA Posta 1018 Dodoma.
Kamanda ZELOTHE STEPEN alipongeza
kitendo Cha kijasiri kilichofanywa na kijana huyo kwa kutambua na kutekeleza
kwa vitendo Mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi
Shirikishi ambao Jeshi la Polisi linahitaji ushirikiano huo sana toka kwa Wananchi
.
“Natoa wito kwa wananchi
wote kuiga mfano wa kijana huyu katika maeneo yenu na kuwa na uchungu dhidi ya watu wasiotaka kufuata sheria, taratibu na kanuni
za usalama barabarani kwa kuwafuatilia na kuwatolea taarifa katika vituo vya Polisi
ili sheria ichukue nafasi dhidi yao” alitoa wito Kamanda Zelothe.
Bw. Zelothe alisema juhudi
za Kulifuatilia gari hilo huku kijana Ally Augustino akiwa amedandia gari hilo
lilihusisha pia mawasilianao na Mtendaji wa kata wa eneo hilo la Chilonwa Bw.
Emanuel Matewa ambaye alichukua hatua kupiga simu kwa walinzi wanaokusanya ushuru wa magari akatika eneo
hilo la Chilonwa ambao nao walidhibiti eneo lao lakini gari hiyo ilipita njia
nyingine.
Aidha Kamanda ZELOTHE
STEPEN alisema mawasilianao yaliendelea kufanyika baina ya Kijana huyo na Askari
wa Wilaya ya Chamwino na Dodoma mjini na
kufanikiwa kulikamata baada ya Dereva kuonyeshwa alama ya kusimama na askari, na
yeye kusimama kisha kufungua mlango na kukimbia kusikojulikana.
Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa
Dodoma alisema gari hilo lilikamatwa maeneo ya Chaduru katika barabara iendayo eneo la Ipagara katika
Wilaya ya Dodoma Mjini na kwamba Jeshi
la Polisi linaendelea kumsaka Dereva wa Gari hilo ili kuweza kumfikisha
mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
Bw. ZELOTHE amesema tayari
maelekezo yameshatolewa kwa Mkuu wa Usalama Barabarani katika Wilaya ya Chamwino
kupitia katika vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika eneo hilo kwenda kumpongeza
kijana huyo na kuwahamasisha wengine waige tabia hiyo ya kishujaa.
No comments:
Post a Comment