MATUKIO KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MJINI MUSOMA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura kulia akiwa na Makamu wa

MGOMO WA WALIMU HAUUSIANI NA MADAI YA NYUMA
Na Shomari Binda
Musoma,
Suala la mgomo wa walimu ulioanza jana Nchi nzima umedaiwa hauusiani
na walimu hao kudai madai ya madeni ya malimbikizo mbalimbali ya miaka
ya nyuma bali yapo masuala mengine ambayo yalipelekea kuwepo kwa mgomo
huo.
Kauli hiyo ilitolewa na kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya
Musoma John Masero alipokuwa akijibu swali la diwani wa kata ya
Nyakato (CCM) ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya Upinzani katika kikao
cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Halimashauri ya Manispaa ya Musoma.
Katika swali lake la
msingi katika kuchangia taarifa ya utekelezaji ya mwaka 2011-2012,Diwani
huyo alitaka kujua sababu zilizopelekea walimu kuingia katika mgomo
ikiwa Halimashauri hiyo haina deni lolote wanalodaiwa na walimu.
Akimjibu Diwani huyo, Masero alisema walimu wamegoma kutokana na
madai ya nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100,nyongeza ya asilimia 55
kwa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi na hisabati pamoja na
nyongezailimia 30 kwa walimu wanaofundisha katika mazingira magumu.
Alidai Halimashauri ya Manispaa ya Musoma ilifanyia kazi agizo la
Serikali katika kuhakiki madai ya walimu nakuwalipa na kufikia hivi sasa
hakuna mwalimu yeyote anayehidai Manispaa hiyo malimbikizo ya madai ya
nyuma.
Alisema kwa sasa hakuna utaratibu wowote wa kufanya
uhamisho kwa walimu kama hakuna fedha za kufanya hivyo ili kuepusha
malimbikizo ya madai yasiyokuwa ya msingi na kujiingiza katika migogoro
isiyo ya lazima baina ya Manispaa na walimu.
Aliongeza kuwa
kutokana na mgomo huo kutohusiana na madai ya madeni ya nyuma suala la
mgomo huo wa walimu unashughulikiwa katika ngazi nyingine zinazohusika
kwa kuwa ni mgomo wa Kitaifa.
Aidha kaimu Mkurugenzi huyo wa
Manispaa ya Musoma amewataka Madiwani kuwashirikisha Wananchi katika
kufanya maandalizi ya kukamilisha baadhi ya maboma ya madarasa kwa ajili
ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza hapo mwakani.
Aidha katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani kimemchagua diwani wa
kata ya Mwisenge (CHADEMA) Bwire Nyamwero kuwa naibu Meya wa
Halimashauri ya Manispaa ya Musoma kuchukua nafasi ya mtangulizi wake
diwani wa kata ya Kamnyonge Angera Lima.
Katika hatua nyingine
Katibu wa Chama Cha Walimu Mkoani Mara (CWT) Fatuma bakari alisema sula
la mgomo ambao wameuanza jana utaendelea kuwepo hadi pale watakapo pata
maelekezo mengine kutoka kwa viongozi wao wa Kitaifa.
BINDA
NEWS liliwashuhudia wanafunzi katika Manispaaya musoma wakicheza nje ya
nadarasa huku wengine wakionekana wakizunguka mitaani kutokanana kile
kinachoonekana walimu kuendelea kuwa katika mgomo.
No comments:
Post a Comment