Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Balozi Khamisi Kagasheki akiwa katika mkutano na wananchi wa Vijiji vitano vinavyounda WMA
Maafisa mbalimbali nao walikuwepo katika mkutano huo uliofanyika jana huko Ikoma
Balozi Khamis Kagasheki akiendelea kutoa somo kwa wananchi
Baada ya mambo mbalimbali baadhi ya wananchi nao walianza kuchangia katika mkutano huo
Baada ya ziara ndefu na kufanya mkutano na wananchi hatimaye Balozi Kagasheki akawa njia kurejea Bungeni mjini Dodoma
Afisa mahusiano wa TANAPA Paschal Shelutete akihakikisha kuondoka kwa Waziri wa Mali Asili
Makamanda wa vita baada ya kuhakikisha wananchi wanapata kila taarifa sasa wakawa
Kama kawa
Viongozi wa jeshi la Polisi wilayani Serengeti wakiteta jambo na wanahabari George Marato na Mabere MakubiWaziri akiwa angani kuelekea mjini Dodoma
SERENGETI
SERIKALI
imesema haitasita kuchukua hatua za kuzifunga kambi zote za kitalii ambazo zimo
katika maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama
pori WMA,ambazo zitaendelea kukiuka sheria na Kanuni kwa kulipa mapato yatokanayo na shughuli ya utalii kwa uongozi
wa vijiji badala ya malipo hayo
kufanyika kupitia WMA.
Agizo hilo
limetolewa na waziri wa Maliasili na Utalii Mh Balozi Khamis Kagasheki,wakati
akizungumza na viongozi wa WMA ya Ikona wadau wa sekta ya utalii katika wilaya
ya Serengeti mkoani Mara.
Amesema hivi
sasa kumeibuka migogoro kwa baadhi ya WMA kwa kuhusisha viongozi na wananchi wa
vijiji husika ambayo imekuwa ikihatarisha amani na mahusiano kati ya kijiji na kijiji
kwa kugombea mapato baada ya baadhi ya kambi za utalii kukiuka kanuni na kwa
kulipa tozo hizo moja kwa moja kwa baadhi ya serikali za vijiji kinyume cha
sheria.
Waziri
Kagasheki,amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mgogoro ambao umekuwa ukiendelea
katika WMA ya Ikona wilayani Serengeti umechangiwa na baadhi ya kambi za
kitalii kulipa mapato yake kwa baadhi ya vijiji wakati wakitambua wazi kuwa
kambi hizo ziko ndani ya eneo la WMA.
Kwa upande
wao baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji vitano vinavyounda WMA ya Ikona,wamesema
mgogoro huo pia umechangiwa na uongozi wa WMA kushindwa kusoma taarifa za mapato
na matumizi kwa wananchi,madiwani kujineemesha huku wananchi wakishindwa kuvuna
mazao mashambani baada ya kushambuliwa
na wanyamapori kutokana tu na kuthamini shughuli za uhifadhi.
WMA ya Ikona
inaundwa na vijiji vya Nyatambiso,Park
Nyigoti,Nyichoka,Makunduzi na Rubanda ambapo tayari WMA 38 zimeanzishwa nchini
17 zikiwa zimetangazwa rasmi katika gazeti la serikali lengo likiwa kuhakikisha
wananchi wanahifadhi na kunufaika na raslimali hiyo kwaajili ya kupunguza
umasikini miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment