MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012 KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA, NA KATI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikiro.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza mgeni rasmi
Afisa Uhamasishaji Said Ameir akitoa Maelezo juu ya Sensa kwa waandishi wa Habari
SENSA-MWANZA
SERIKALI imesema kuwa haitamvumilia mtu yeyote
atakayeingiza sula la itikadi za kisiasa na imani za kidini katika zoezi la
sensa na makazi linalotarajia kuanza Augost 26 mwaka huu.
Akifungua semina ya siku mbili kwa waandishi wa
habari kutoka mikoa kumi ya kanda ya ziwa na kanda ya kati,mkuu wa mkoa wa
Mwanza Injinia Everist Ndikilo amesema kuwa vyombo vya habari vinajukumu kubwa
katika kufanikisha zoezi la Sensa na makazi linafanikiwa.
Amesema jukumu kubwa la vyombo vya habari katika zoezi
la Sensa ni kuelimisha,kuhabarisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika
zoezi hilo litakapoanza.
Injia Ndikilo amesema kuwa taarifa zote
zitakazopatikana katika zoezi hilo zitakuwa siri huku akisema kuwa zoezi hilo
halitahathiri shughuli za kiuchumi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika semina hiyo,
Afisa uhamasishaji Said Ameir amesema
kuwa sekta ya habari ni miongoni mwa wadau wakubwa katika zoezi la Sensa huku
akisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi inayofanya zoezi la Sensa kwa ubora.
Zoezi la Sensa na Makazi linatarajiwa kufanyika Agost 26 huku wananchi wakihimizwa
kuwa zoezi hilo ndilo litasaidia katika mipango ya Maendeleo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment