Saturday, May 21, 2011
WANANCHI WA TARIME WATAKA MKUU WA WILAYA NA KAMANDA WA KANDA MAALUM YA KIPOLISI WAACHIE NGA
WANANCHI wilayani Tarime mkoani Mara wamewataka mkuu wa wilaya hiyo John Henjewele pamoja na kamanda wa polisi wa kandada maalumu Tarime/Rorya kujihuzulu nyadhifa zao katika kurejesha amani wilayani humo.
Wananchi hao wameyasema hayo wakati walipokuwa wakihojiwa na wanasheria wa shirika lisilo la kiserikali kutoka kituo cha haki za bianadamu kuhusiana na matukio ya kinyanyasaji yanayotokea katika wilaya hiyo mara kwa mara.
Wananchi hao ambao wengi wao ni ndugu wa marehemu waliouawa Mei 16 mwaka huu ambapo wamesema kuwa ndugu zao wengi walikwisha uawa kwa shinikizo la kuhusiana na mgodi huo wa dhahabu wa north Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gald.
Hata hivyo wamesema lengo la kuwakataa viongozi hao ni pale wanapothamini maslahi yao binafsi na kuona raia wa kawaida kama mnyama ambaye hana thamani yoyote.
Wamesema kila kunapotokea matatizo kuhusu mgodi huo wanachi wanakuwa mstari wa mbele kwenda kwa mkuu wa wilaya kutoa taarifa lakini mkuu huyo amekuwa akiwapa majibu yanayokatisha tama,kana kwamba wao sio watanzania ni wavamizi.
Kuhusu kamanda wa jeshi la polisi wamedai kuwa kamanda huyo amekuwa akiyafumbia macho mauaji yanayofanywa na jeshi hilo ovyo ovyo,pamoja na kuwabambikizia kesi vijana wanaooneka kufuatilia haki kwa jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment