SERIKALI imewataka Watanzania kuenzi Utamaduni ambao utakua kichocheo za kuzuia maovu ndani ya jamii hasa katika vita dhidi ya vitendo vya Rushwa,Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto,Ujambazi,Uporaji na Mauji ya kinyama ambayo yamekuwa yakifanywa kwa imani potofu.
Waziri wa habari,vijana utamaduni na michezo Mh Dk Emanuel Nchimbi,ametoa kauli hiyo mjini musoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya utamadini duniani, ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara.
Amesema ni imani yake kuwa endapo kila mtu atauenzi utamaduni wake hakutakuwepo mambo hayo maovu ndani ya jamii hivyo kuwataka watanzania kutafakari kwa kina maovu hayo kwa kuachana nayo ili amani na utulivu viimarike na kutawala hapa nchini.
Mh Dk Nchimbi,amesema mila na desturi zikitumika vizuri ni ukweli zitasisitiza kufanya kazi kwa bidii,kuzalisha mali,kuheshimu madaraka na mengine mengi na hivyo kuliwezesha taifa kusonga mbele kwa kila Nyanja kikiwemo kilimo na kuhakikisha nchi inakidhi kwa mahitaji yake hasa chakula.
Kw upande wake katibu mkuu wa wizara ya habari,vijana,utamaduni na michezo, Bw Sethi Kamuando,akizungumza katika kilele hicho amesema hivi sasa kumeibuka kundi la baadhi ya viongozi wa siasa ambao wamekuwa wakitumia mgongo huo kuwagawa wananchi jambo ambalo amesema ni dalili mbaya zinazotishia umoja na mshakamano nchini.
Kilele hicho chenye kauli mbiu TUSHEREKEAPO MIAKA 50 YA UHURU TUDUMISHE UTAMADUNI WETU,zimefanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment