Friday, May 6, 2011

KUPUUZA KAULI ZA VIONGOZI SI JAMBO JEMA

Bukoba

WAFANYABIASHARA wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wanadaiwa kupuuza agizo la waziri mkuu Mizengo Peter Pinda lilowataka washusha bei ya Sukari kutoka shilingi 2,200 hadi shilingi 1700 kwa kilo moja.

Mwezi mmoja uliopita waziri mkuu akiwa ziarani mkoani Kagera,alionekana kushutushwa kwa kupanda kwa bei ya sukari wakati bidhaa hiyo ikizaliwashwa mkoani humo hivyo kuwataka wafanyabishara kushusha haraka bei hiyo na viongozi kusimamia suala hilo ili kuondoa dhuluma hiyo kwa wananchi.
Wazee wa mkoa wa Kagera,waliyasema hayo juzi wakati wakizungumza na waziri wa nchi ofisi ya rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wassira,katika mkutano ambao umeitishwa na kiongozi huyo kwaajili ya kuzungumzia msuala mbalimbali yanayolikabili taifa kwa hivi sasa.

Mmoja wa wazee hao wa mji wa Bukoba  Richard Emanuel,akizungumza katika mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera,alisema licha ya waziri mkuu kutangaza kushushwa kwa bei ya sukari kutoka 2,200 hadi 1700 kwa kilo lakini hadi sasa agizo hilo linaonekana kupuuzwa na  wafanyabiashara hao huku vingozi wa wilaya na mkoa wakishindwa kuchukua hatua.

“Tunataka kujua ni kwanini viongozi nyinyi hasa rais na waziri mkuu wakitoa maagizo yanaonekana kupuuzwa sana na watu huku viongozi wa chini ambao ni watendaji wakishindwa kuchukua hatua..kwa mfano juzi waziri mkuu alisema sukari ishuke lakini hadi sasa bei ni ileile ya shilingi 2,200 sasa sisi wananchi tutawaelewaje?”alihoji mzee huyo.

Hata hivyo wazee hao,waliiomba serikali kufikiria sasa namna ya kudhibiti mfumuko wa bei unalikabilia taifa ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa bidhaa muhumu zinazotumiwa kila siku na wananchi yakiwemo mafuta na chakula ili kuwapunguzia makali ya maisha kwa wananchi.

Walisema kuwa hivi sasa tangu kutangazwa kupanda kwa bei ya mafuta kumetokea mfumuko mkubwa na wa ajabu kwa kupanda kwa bidhaa muhimu kikiwemo chakula jambo ambalo linameongeza ughali wa maisha kwa wananchi.

“Hatuwezi kusema tudumishe amani wakati wananchi wanakabiliwa na matatizo rukuki sasa sisi wazee wa bukoba tunaiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku kwa bidhaa mihimu ili kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi”alisema mzee Saimon Mlokozi.

Akizungumzia kuhusu kupuuzwa kwa agizo la waziri mkuu,mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu,pamoja na kukiri kuwa bado kuna idadi ya wafanyabiashara ambao wamekaidia agizo hilo,aliwaagiza viongozi wa wilaya na halmashauri kuendesha msako mkali katika maduka ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kuwafungia leseni wafanyabiashara wote watakaobainika kuendelea kuuza bidhaa hiyo kwa shilingi 2,200 kwa kilo.

“Waziri mkuu alikutana na wauzaji wa bidhaa hii na kukubalina kupunguza sukari hadi 1700 kwa kilo wapo ambao wamefanya hivyo lakini wapo ambao wameonekana kukaidi agizo hili sasa nawaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuendesha msako mkali na ikibidi kufungiwa leseni za kufanyabiashara hiyo maisha”alisema RC Babu.

Kwa upande waziri Wassira,iliwaomba wazee na viongozi wa dini mkoani Kagera, kukemea watu ama chama chochote cha siasa nchini chenye dalili za kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini,ukabila na ukanda kwa vile kundekeza vitendo hivyo vinaweza kuchochea chuki na kuhatarisha amani ya nchi.

Wassira alisema hayo kwa nyakati tofauti wakati akiongea na wazee wa mji wa Bukoba pamoja na viongozi wa dini wa mkoa wa Kagera.

Alisema kuna baadhi ya watu wakiwemo viongozi na vyama vya siasa wamekuwa wakitumia matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa hivi sasa kwaajili ya kujaribu kuichonganisha serikali na wananchi wake jambo ambalo amesema si sahihi kwani kufanya hivyo kunaweza kuvuruga umoja na mshikamano wa watanzania ambao umewezesha kufikia miaka 50 ya uhuru.

Waziri huyo wa nchi ofisi ya rais mahusiano na uratibu,alisema serikali ingependa kupata mawazo mbadala kutoka kwa watu,viongozi wa vyama vya siasa na wale wa dini kwa misingi ya kujenga nchi lakini si kuleta chuki kati ya wananchi na serikali yao.

“Sisi kama serikali hatukatai ushauri kwa kujenga nchi lakini si kutumia matatizo ambayo yanatokana na mafanikio kuichonganisha seikali na wananchi wao ..kuanzisha vyama  vya siasa lengo kubwa ni kuikumbusha serikali iliyopo madarakani si kuleta chuki ama ukitaka kuipindua hii hawezekani”alisema Waziri Wassira.

Kuhusu suala la mchakato wa katiba mpya, Waziri Wassira aliwataka viongozi wa siasa na viongozi wa dini kuelimisha wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni wakati wote wa mchakato huo ambayo yatawezesha kupatukana kwa katiba mpya kwa njia ya amani na utulivu.

Mwisho

No comments:

Post a Comment