Friday, February 4, 2011

TAKUKURU WATAKIWA KUFANYA UCHUNGUZI

Musoma
 
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilaya Rorya mkoani Mara imeombwa kufanya uchunguzi wa kina juu ya baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo ambao wamekuwa wakitumia mamilioni ya fedha kila mwezi kwaajili ya kulipia gharama za hoteli katika wilayani Tarime.
Imedaiwa kuwa watumishi hao wamekuwa wakifanya kazi katika wilaya ya Rorya na baada ya muda wa kazi ulazimika kusafiri kwa usafiri wa ofisi ama binafsi hadi wilayani tarime na kulala katika nyumba za wageni kwa kisingizio cha kukosa nyumba za kuishi wilayani Rorya.
Habari kutoka Rorya zinadai kuwa zaidi ya watumishi sita wa idara mbalimbali ikiwemo ya fedha kwa zaidi ya miezi sita sasa wamekuwa wakiishi katika nyumba za kulala wageni wilayani Tarime kwa kulipa  wastani wa milioni 1.6 kwa mwezi huku mishahara yao ikitajwa kuwa chini ya milioni 1.3 kwa mwezi.
Baadhi ya hoteli wanazoishi  watumishi hao ni Free zone ambapo wamekuwa walipa wastani wa shilingi 35,000 kwa siku kwaajili ya malazi na chakula huku watumishi wengine wakiishi hotel ya Mac ambayo pia wamekuwa wakitumia wastani wa shilingi 38,000 kila siku.
Hata hivyo haijajulikana wazi kuwa endapo fedha hizo zinalipwa na uongozi wa halmashauri kwa fedha za walipa kodi ama kupitia mishahara yao ingawa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ernest Basaya alikiri kuwa mweka hazina wake ni miongoni mwa watu walikuwa wakifikia hoteli.
“Mimi ambacho najua wakati mweka hazina ameripo hapa halmashauri kweli alienda kupanga hotelini na mimi kwa mujibu wa kanuni za fedha nilimlipa malipo ya siku 14 pamoja na hela za mizigo sasa kuanzia hapo kama bado yuko hotelini labda anatumia fedha zake”alisema Basaya na kuongeza.
“Lakini nadhani wanaishi hotelini kwa vile hapa rorya kila kukicha wanapandisha kodi za nyumba sasa tunona ni vema tuishi tarime kuliko hapa hata hawa wenye nyumba wana mpango wa kuzirejesha ili wote waende tarime na hivi sasa nina pango wa kukutana na viongozi wenzangu tuone jinsi ya kuzungumza na wenye nyumba kuona namna ya kupunguza kodi hizi”alisema.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa tayari baadhi ya wananchi wa wilaya ya rorya wamepeleka malalamiko yao takukuru dhidi ya watumishi hao kulalamikia kuishi kwao nje ya vituo vyao vya kazi ambapo walisema licha ya kuchelewa wakati mwingine kufika maofisini kwaajili kutoa huduma  lakini pia wamekuwa wakitumia vibaya raslimali za halmashauri kwaajili ya usafiri wa kwenda na kurudi kila siku kutoka rorya hadi tarime.
“Hapa kuna ufisadi wa kutisha haiwezekani watu wakaacha ntumba hapa rorya wakaenda kuishi tarime kwa fedha za nani haiwezekani mtumishi utumia mshahara wote kulipia kodi ya nyumba je wao hawana familia lazima takukuru ifanye uchunguzi wa kina kujua vyanzo vyao vingine vya mapato yao mbali na mshahara ambao hautoshi hata kulipiagharama hizo”alisema mmoja wa mmtumishi wa idara ya fedha jina tunalo(Charles Marwa).
Kwa mujibu wa habari hizo kuwa kwa kipindi hicho cha miezi sita tayari watumishi hao wametumia zaidi ya milioni 40 kwaaliji ya gharama za chakula na malazi mbali na mafuta yanayotumika kwaajili ya usafiri wa kila siku wa kutoka tarime na rorya.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Charles Ochere,alikiri kuwepo kwa watumishi wanaoshi nje ya vituo vya vya kazi akiwemo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo na kusema tayari suala hilo limelizungumzwa katika kikao cha waziri wa ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma  Hawa Ghasia ambaye alitaka watumishi hao kuama wilayani tarime.
“Hili jambo juzi pia lilizungumzwa katika kikao cha waziri Ghasia kwani mbali na watumishi hao kuishi hotelini hata mkurugenzi mwenyewe anaishi tarime wakati hapa kuna nyumba sasa wamekuwa wakiingizi halmashari yetu gharama kubwa”alisema Ochere.
Alisema si kweli kuwa kodi za nyumba wilaya ya rorya ziko juu kama wanavyodai kwa maelezo kuwa baada ya kutolewa kwa hoja hiyo aliwataka watumishi wanaodai kupandishiwa kodi hizo kujitokeza lakini hakuna hata mmoja aliyefanya hivyo.
Akizungumza na nipashe kwa njia ya simu mmoja ya watumishi hao ambaye ni mkuu wa idara ya fedha Caisari Ninalwo,alisema kuishi kwake hotelini ni suala binafsi ambalo halipaswi kuingiliwa hata kama zinazotumika ni fedha za walipa kodi.
“Kama naishi hapa hotelini wewe kinakuuma nini kwani wewe ndo unalipa inawezekana nalipa kwa fedha zangu ama halmashauri inalipa lakini wananchi wa rorya hawajalalamika wewe kinakuuma nini”alisema.

               MBUNGE AFANYA KUFURU
Rorya
Ikiwa  ni miezi mitatu tu tangu wabunge wapya wa bunge la kumi waapishwe kushika nyadhifa hizo mbunge mmoja wa chama cha mapinduzi amefanya kufuru kwa kutekeleza miradi ya zaidi ya shilingi milioni mia tano kwa kipindi hicho.
Mbunge huyo wa jimbo la Rorya Lameck Airo maarufu kama profesa huruma,ameweza kutekeleza miradi hiyo ya sekta ya elimu,afya,maji,barabara na miradi mingine ya kiuchumi kwa kugharimu zaidi ya milioni mia tano.
Katika ujenzi wa ukarabati wa barabara mbunge huyo tayari amenunua grada kwa kiasi cha zaidi ya milioni 280 ambayo itatumika kufungua barabara zote za jimbo hilo na kuwezesha kupita kwa muda wote na hivyo kurahisisha usafiri na kushuka kwa gharama za nauli.
Alikizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 34 ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya rorya katika kijiji cha Ochuna,mbunge huyo alisema kwa kutumia mkopo wa fedha kwaajili kununulia gari la ubunge ameweza kutumia fedha hizo kununulia greda hilo ili kusadia ujenzi wa barabara za jimbo hilo ambapo halmashauri ya wilaya ya rorya imekubali kugharimia mafuta kwaajili ya kazi hiyo.
“Mimi nilisema sitaki ubunge kwaajili ya manufaa yangu bali nilitaka nafasi hii ili name nipate nafasi ya kuchangia maendeleo ya jimbo langu ndio maana fedha za kununulia shangingi la ubunge mimi nimezipeka kununulia grada litakalosadia ujenzi wa barabara zote ndani ya jimbo”alisema Airo huku akishangiliwa.
Alisema wakati akiomba kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana alishuhudia idadi kubwa ya watoto wa shule za msingi wakisoma huku wakiwa wamekaa chini ya sakafu na hivyo kuamua kutumia zaidi ya milioni 130 kwaajili ya kutengeneza madawati zaidi ya 2,600 ambayo tayari yameanza kusambazwa katika shule hizo katika kukabiliana na tatizo hilo.
“Mimi na baadhi ya marafiki zangu tayari nimekamilisha utengenezaji wa madawati zaidi ya 2600 ambayo sasa yanasambazwa katika shule zetu na ninaamini kwa kipindi kifupi tatizo hilo katika shule zetu litakuwa ni historia”alisema.
Hata hivyo mbunge huyo ambaye ndiye alimwangusha baba yake mdogo katika kura za maoni Prof Phillemon Sarungi,alisema endapo mwenyezi mungu atampa uzima anatarajia kukamilisha ahadi zote ndani ya jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu tu kuanzia sasa.
Akiwa katika ziara katika kijiji cha Bwiri,mbunge huyo alichangia zaidi milioni 30 kwaajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu katika shule hiyo baada ya kukuta watoto wakisoma chini ya mti.
Aidha akiwa katika kijiji cha Ikoma mbunge huyo alichangia mbao,nondo na saruji kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya mganga huku akihimiza wananchi kutumia uwezo walionao kuchangia miradi ya maendeleo na kwamba yeye kama mbunge ataunga mkono juhudi hizo za wananchi.
Hata hivyo mbunge huyo alipongezwa na wananchi wa kijiji cha Buganjo kwa kuwajengea daraja katika mto mori ambapo aliwesema tangu nchi upate uhuru wamekuwa wakitoa kilio cha kujengewa daraja hilo serikalini na kwa wabunge waliomtangulia lakini wamekuwa hawatekelezi na hivyo kuwakwamisha shughuli zao za kilimo wakati wa masika kwa kushindwa kuvuka eneo hilo.
Katika kukabiliana na tatizo la uharamia ndani ya ziwa Victoria ambalo limekuwa likiwakumba wavuvi wa Tanzania kwa kuvamiwa na watu wanaodaiwa ni askari jeshi kutoka nchini Uganda mvuvi huo ametoa msaada wa boti iendayo kasi ili kuwezesha polisi wa kikosi cha majini cha sota wilayani rorya kufanya doria hiyo usiku na mchana katika kuokoa maisha na mali za wavuvi hao.

No comments:

Post a Comment