Wednesday, January 19, 2011

TISA WACHARAZWA MAPANGA MUSOMA

MUSOMA

WATU tisa wamekatwa mapanga sehemu mbalimbali ya miili yao jana majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Mkirira kata ya Kigera Etuma katika halmashauri ya Musoma mkoani Mara.

Wakiongea katika hospital ya mkoa wa Mara majeruhi hao walisema kuwa  wahusika wa tukio hilo ambao walikuwa na mapanga,sime na Marungu hawakuwezakufahamika  mara moja wakati wanafanya tukio hilo.

Tukio hilo ambalo lilitokea katika barabara ya Mkirira kwa wavamizi hao kuweka mawe barabarani na kisha kuteka watu waliokuwa wakipita eneo hilo na kuwapora kila kitu walichokunacho.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Kamishina msaidizi ACP Robert Boaz alisema katika utekaji huo pikipiki tano zilitekwa,baiskel nne na gari moja aina ya Fuso lenye namaba za usajili T174 AAI lililokuwalikiendeshwa na dreva aliyefahamika kwa jina la Kisukari Yahya ambaye aliporwa kiasi cha shilingi milioni moja na laki sita.

Akiwataja watu wengine waliokumbwa katika tukio hilo ni pamoja na Suleman  Mrutu ambaye ni dreva wa bodaboda,Wilson Kaiza,Charles Philimo,Jumbe Ally ambaye kwa sasa hali yake ni mbaya.

Wengine ni Gorio Msira,Eliza Michael na Didas Vicent,Kamanda Boaz alisema kuwa baada ya tukio hilo majambazi hao walitokomea sehemu isiyofahamiaka na kuziacha Pikipiki,Baiskael na Gari katika eneo la tukio huku wakiondokana na fedha pamoja na Simu.

No comments:

Post a Comment