Saturday, January 22, 2011

SASA HII KALI NADHANI NI YA KWANZA NCHINI

Jana Mh Nyerere alikutana na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia jimbo la Musoma mjini kwa tiketi ya chama cha DP Ndege Nyakitita na kumrudishia kiasi cha shilingi elfu 50000 ambazo alitumia wakati wa uchaguzi kuchukua fomu.Nyerere alisema na hiyo atafanya kwa kila mgombea aliyeshindwa kwani hataki kumsababishia mtu maumivu ya moyo kwa fedha aliyotumia kipindi hicho

 Mh mbunge akihesabu kiasi cha shilingi elfu 50000 kumkabidhi Nyakitita kama ishara ya kumrudishia fedha alizotumia kuchukua fomu wakati wa uchaguzi.Wakati anapokea Nyakitita alisema hiyo ni ishara nzuri kwa kuthamini wenzake

 Hapa jamaa anakabidhiwa fedha kama kamera yangu ilivyonasa vyema
Shukrani ni muhimu kwa kila jambo,Nyakitita akishukuru baada ya kupewa fedha hizo

No comments:

Post a Comment