Wednesday, January 19, 2011

MTOTO WA MWAKA MMOJA ABAKWA MUSOMA

 
Mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitatu amebakwa na kijana wa miaka wa miaka 28 katika kata Makoko manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Tukio hilo lilitokea January 15 mwaka huu majira ya saa nane mchana ambapo mama mzazi wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Nyamsola Masige amesema siku ya tuki hilo alimwacha mtoto huyo na bibi yake huku yeye akielekea msibani.

Alisema wajira ya saa nane wakati akirejea nyumbani alikuta umati mkubwa wa tu wakiwa nyumbani kwakwe na baada ya kifika ndipo alipoambiwa kuwa mwanae amebakwa na kijana aliyefahamika kwa jina la Paul Manoko anayeishi katika nyumba hiyo ambaye ni ndugu yake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi ACP ROBERT BOAZ  na mtuhumiwa huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mara.

No comments:

Post a Comment