Thursday, January 20, 2011

MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI ATEMBELEA WAGONJWA NA KUTOA VITABU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARY KATIKA JIMBO HILO

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vincent Nyerere leo ametembelea wagonjwa katika Hospital ya Mkoa wa Mara ambapo baadhi yao walitekwa na kukatwa mapanga juzi.

Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo ambaye ni mmoja ya wahanga ambao walitekwa na majambazi kisha kunyang'anywa fedha na mali zao

Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo,mzee huyu ana umri wa miaka 67 lakini cha ajabu ameshindwa kupata huduma stahiki kwa kile kinachosemekana hana fedha lakini wadau sera ya wazee inasemeaje? kilio chake kimefika kwa mheshimiwa Nyerere 

Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo,huyu aliwahi kuwa katibu wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na katika maelezo yake anasema kuwa majambazi waliomvamia kwake walikuwa zaidi ya nane na walipofanikiwa kuingia walimkata panga kama uonavyo picha hiyo na kisha kuchukua redio na fedha kiasi cha laki nane lakini baadaye redio zilipatikana maeneo ya uwanja wa ndege

Hivi ni vitabu ambavyo vilitolewa na mheshimiwa mbunge wa jimbo Musoma mjini Vincent Nyerere  katika kusaidia sekta ya elimu ndani ya jimbo la Musoma mjini
Waswahili nanasema elimu ndio msingi wa maisha ya mtanzania na ndio itakuwa dira nzuri katika kuondoa umaskini jimboni Musoma
  Walimu wa shule mbalimbali katika jimbo la Musoma mjini wakiangalia vitabu ambavyo vimeletwa na mbunge wa jimbo hilo
 Baada ya kuwa katika viwanja vya  Manispaa ya Musoma mara akatokea Afisa Utamaduni katika manispaa hiyo Shekdad na kuanza kulonga juu ya vitabu hivyo na suala zima la michezo
          Maelezo bado yanaendelea kati ya afisa utamaduni na Mheshimiwa Nyerere
    Mashuhuda katika ugawaji wa vitabu hivyo walikuwepo kama wanavyoonekana Mwarabu kushoto ambaye ni mpiga picha wa ITV na mtangazaji kutoka Victoria fm ya mjini Musoma
                                      Elimu Kwanza
Nami nilipata nafasi ya kubadilishana mawazo na Afisa utamaduni Manispaa kuhusu masuala ya kimichezo katika manispaa hiyo,mbali na hapo alikuwa akipongeza kauli ya mbunge juu ya dhamira yake ya kuendeleza michezo

No comments:

Post a Comment