Saturday, January 22, 2011

JANA MH NYERERE ALITEMBELEA KIWANDA CHA MUTEX MUSOMA

 Kiwanda cha nguo cha Mutex ni kiwanda kikongwe Afrika Mashariki lakini kinaonekana kama ndio kinakufa hivyo,jana Mh Nyerere alifanya ziara katika kiwanda hicho lakini hali inaonekana kuwa tete kwani kila mashine tuliyouliza jibu lilikuwa hiyo ni mpya.swali je za zamani ziko wapi ? mwekezaji Mhindi kweli jamani?
 Hili ni vumbi ambalo Mh Mbunge alisema liondolewe kwa sababu linaathiri wanafunzi wa shule ya sekondary Musoma Tech wakati upepo ukivuma kuelekea upande wa shule hiyo
 Hizi mashine zinaonekana kama vyuma chakavu
 Jamani kweli kiwanda kiliendeshwa kwa stahili hii ya mashudu?
 Tazama uharibifu huu wa misitu?raia wa kawaida wanaotumia kwa ajili ya kupika tunasema wanaharibu mazingira je na hawa wanafanya nini?
 Mh Nyerere akitazama mfereji wa maji machafu yanayotoka kiwandani yakielekea ziwani ingawa wahindi hao walikataa lakini ukweli yanaelekea ziwa Victoria
 Sehemu hiyo inaonekana imezibwa ili maji yaelekea sehemu ambayo haikustahili,pamoja na hivyo kiwanda hicho kina wafanyakazi wasiozidi 50 je hayo maji yanaathiri watu wangapi?
 Hizi ni mashine ambazo wanasema wameleta ili kufufua kiwanda hicho je itawezekana ?
 Mashine za hapa zilienda wapi?
 
 

No comments:

Post a Comment