Monday, January 31, 2011

IDARA YA ARDHI MANISPAA YA MUSOMA WAHUSIKA KWA MIGOGORO


WAKAZI wa manispaa ya Musoma mkoani Mara wanailalamikia idara ya ardhi katika halimashauri hiyo kwa kuchangia migogoro mingi ya aridhi kwa kile walichodai kuwa kiwanja kimoja humilikiwa na watu zaidi ya wawili.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya ofisi ya ardhi katika manispaa hiyo wananchi hao ambao hawakupenda majina yao kutajwa gazetini walisema kuwa idara hiyo imekuwa ikitoa idhini ya kumiliki kiwanja kwa wananchi zaidi ya mmoja huku ikigundulika kuwa wamefanya hivyo hukana kwa kusema hawausiki

Katika sakata hilo ambalo linaonekana kero katika manispaa hiyo kwa wananchi waliongeza kuwa mbali na viwanja hivyo kugawiwa mara mbili kwa wananchi lakini bado idara hiyo imekuwa kero katika suala zima la rushwa,alisema kuwa amekuwa akilipia kodi kiwanja chake  kilichopo katika kata ya Bweri eneo la Mutex tangu mwaka 2004.

Mwananchi huyo alisema kuwa ilipofika mwaka 2009 alipata safari baada ya kurudi mwaka Novemba  2010 na alipoenda kulipia kodi ya kiwanja alibaini kuwa kuna mtu mwingine anaelipia kiwanja hicho na kwamba mtu huyo alikuwa tayari alikwishapewa ruhusa ya kujenga katika eneo hilo.

 ‘Mimi nilikuwa nimesafiri na niliporudi mwaka 2009 nikaja manispaa kulipa kodi ya kiwanja cha ajabu nilipofika wanasema eti kiwanja hicho kuna mtu analipia,jamani sasa huu kweli ni ungwana? Alisema mama huyo

Mama huyo alisema kuwa baada ya kubaini tatizo hilo alijaribu kuuliza akaambiwa aandike barua ya malalamiko kwa afisa ardhi ili aweze kulishughulikia ambapo alisema kuwa alifanya hivyo lakini mizunguko ndio ikawa mingi.

Aidha mwananchi mwingine ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Dereck Murusuri alisema kuwa alinunua kiwanja mwaka 2010 katika kata ya Kigera  kutoka kwa Idirisa ambae alimweleza kuwa kiwanja hicho ni chake hivyo akamuuzia kiwanja hicho Bloc Y namba 77.

Alisema kuwa kabla ya kununua alifuata taratibu zote katika ofisi ya manispaa hiyo katika ununuzi wa kiwanja hicho na kuthibitishiwa na afisa ardhi ambaye alisema kuwa kiwanja hicho ni cha Idrisa.

‘Kwanza kabla sijanunua nilifuata taratibu zote katika ofisi ya ardhi manispaa ya Musoma na wao wakathibitisha kuwa kiwanja hicho ni cha Idrisa lakini baadaye mwenye kiwanja akajitokeza,sasa ungwana upo katika hilo” alihoji Murusuri

Murusuri alisema kuwa baada ya kununua kiwanja hicho alianza taratibu za kujenga lakini wakati akifanya hivyo alijitokeza mtu mwingine aliyemtaja kwa jina mmoja Mariamu akidai kuwa kiwanja hicho ni chake

Alisema baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa kiwanja hicho alichouziwa kilikuwa na mgogoro wa kifamiliya na kwamba aliyemuuzia kiwanja hicho alitumia nyaraka batili.

Kwa upande wake afisa ardhi Daudi Magabe alipoulizwa juu ya suala hilo na malalamiko mengine ya wananchi alisema kuwa malalamiko ya viwanja ni mengi katika ofisi yake kwa kuwa watu wengi hununua viwanja bila kufanya upembuzi yakinifu.

Aidha akitolea mfano kiwanja hicho cha Kigera Block Y namba 77 afisa huyo alisema muuzaji alikuwa na nyaraka zote ambazo alitokanazo mahakamni zikionyesha kuwa yeye ndiye mmili halali wa kiwanja hicho alichokusudia kuuza kwa Murusuri.

Katika sakata hilo la kiwanja hicho cha Kigera Bloc Y 77 ambapoMugabe alisema kuwa kiwanja hicho kimebainikakuwa aliyekinunua alitapeliwa hivyo ofisi ipo katika utaratibu wa kumtafuta aliyeuza kiwanja hicho ili achukuliwe hatua za kisheria

Alipoulizwa ni kwanini ofisi yake ilikubali kupokea nyaraka batili wakati wa kuuza kiwanja hicho alisema kuwa ofisi yake imebaini kuwa kiwanja hicho kina mgogoro wa kifamilia.

Aliongeza kuwa kiwanja hicho kitabaki kuwa cha aliyekuwa akikimiliki mwanzo na huyo aliyeuziwa atalazimika kumtafuta aliyemuuzia ili amrudishie fedha zake.

Naye mkurugenzi wa halimashauri hiyo Nathani Mshana alisema kuwa kuhusu matatizo ya aridhi katika halimashauri hiyo ni mengi hali inayoonekana kuwa kitovu cha mgogoro wa mda mrefu .

Mshana alisema uchunguzi uliofanywa na halimashauri hiyo ulibaini kuwa baadhi ya migogoro inachangiwa na vijana waliokuwa wameajiriwa na manispaa kwa ajili ya upimaji wa viwanja baada ya maafisa aridhi kuoneka kuwa na kazi nyingi.

Alisema vijana hao kwa hivi sasa wameachishwa kazi wote na kazi zote za upimaji wa aridhi zinatakiwa kufanywa na afisa aridhi mwenyewe hata kama kazi ni nyingi.

Akiongea kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mheshimiwa Vincent Nyerere alisema kuwa suala la migogoro katika viwanja ni la muda mrefu katika jimbo la Musoma mjini hivyo ofisi yake imejipanga kutatua mzozo huo

Alisema zipo taarifa za kuwepo kwa harufu ya rushwa katika ofisi hiyo hivyo atakaa na watendaji wengine wa ofisi ya ardhi ili kujua ni jinsi gani watatatua migogoro hiyo

No comments:

Post a Comment