Friday, December 17, 2010

WAKUFUNZI WA St AUGUSTINE WALIOTOA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA VICTORIA FM

 Huyu anaitwa Bi Getruda John ni mkufunzi katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine ametoa mafunzo kuhusu mambo ya utangazaji na uandaaji wa vipindi katika Redio(Preparation of Radio Program)


Anaitwa Bi Abishagi Bhoke ambaye  pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Mt Augustine cha jijini Mwanza ambaye yeye katika mafunzo haya alifundisha jinsi ya mwandishi wa habari hasa katika redio kuwa na ushawishi kwa wasikilizaji wake( Art of Persuasive Communication)

 Huyu anaitwa Mr Denis Mpagaze ni mmoja wa wakufunzi katika chuo kikuu cha Mt Augustine cha jijini Mwanza na pia ameweza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Victoria Fm katika suala zima maadili ya uandishi wa habari(Journalism Ethics)

 Anaitwa Mr Lubaba naye  ni mkufunzi katika chuo kukuu cha Mt Augustine ambaye yeye katika mafunzo hayo alifundisha kuhusu habari za uchunguzi( Investigative Journalism)
 Anaitwa Mr Paschal Shao ni mkufunzi pia katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine,katika mafunzo hayo alihusika katika mafunzo ya utatuzi wa migogoro(Mediatory report and Conflict Resolution).
Huyu ni Mr Masanja ambaye pia ni mhadhiri katika chuo hicho na katika mafunzo hayo alifundisha kuhusu sheria za mambo ya habari(Journalism laws)

No comments:

Post a Comment