Friday, December 31, 2010

HAPPY NEW YEAR 2011

Mdau habari za kazi,natumaini u mzima katika mikikimikiki ya kutafuta maisha na natumaini si haba Mola anajalia,Leo majira ya saa sita tutakuwa tumeingia katika mwaka mpya kabisa wa 2011 lakini je Malengo yako ya mwaka 2010 yamtimia? Ndio swali ambalo nadahani kila mmoja anapaswa kujiuliza. Pamoja na kujiuliza swali hilo lakini si mbaya ukaweka mipango ya mwaka 2011 kwani siku 365 ni chache katika kutafuta.

Namshukuru Mungu kwani yale yote ambayo nilikuwa nimepanga kwa mwaka 2010 nimefanikiwa kwa asilimi 85 na tayari nimeishajua nini ambacho kilifanya nifikie lengo la asilimia mia moja. Mipango ni mengi na kila mtu anamuomba Mungu lakini naomba usichoke kulitaja jina la bwana.

Najua katika blog hii kuna mengi mnakosa lakini naomba radhi maana hata Roma haikujengwa kwa siku  moja,pamoja na hayo lakini pia nakushukuru sana wewe mdau kwa kuniunga mkono katika kutazama blog hii ya Mwanawaafrika na kuweza kupata marafiki kutoka nchi mbalimbali


Mwaka wa 2011 natumaini kila mtu ameupanga kuwa mwaka wa mafanikio kwakwe blog hii inakutakia mafanikio mema mdau wangu

Nakutakia Mwaka mpya wenye mafanikio na Mola akulinde mdau wangu tuonane tena mwakani.

                                                Nakutaki heri na fanaka ya mwa 2011
                                                   Augustine Boniphace Mgendi(Mwana wa Afrika)
                                                       Mmiliki wa blog ya Mwanawaafrika 

No comments:

Post a Comment