WAFANYABIASHARA MUSOMA WAILALAMIKIA
MANISPAA YA MUSOMA
Augustine Mgendi
MUSOMA
Wafanyabiashra wa Soko la Mwigobero
Manispaa ya Musoma mkoani Mara wameulalamikia
uongozi wa Manispaa hiyo kutaka kuwaondoa katika Soko hilo bila
kuwatengenea Maeneo Mengine ya kufanyia Biashara Zao
Wakiongea kwa Nyakati tofauti katika
eneo la Soko hilo la Mwigobero,Wafanyabiashara hao walisema kuwa eneo hilo
limekuwa msaada mkubwa katika kuendesha Maisha yao ya kila siku katika eneo
hilo.
Walisema Uongozi wa Manispaa umeshindwa
kuwaweka wazi ni wapi wataelekea baada ya kuondolewa katika eneo hilo na hivyo
kuendelea kufanyabiashara bila kujua hatima yao.
“Mpaka sasa ndugu yangu hatujui wapi
tutaenda Maana naona kama hawa Manispaa wanataka kutuhatarishia Maisha yetu na
Familia zetu,hapa ndipo tunapata Chakula chetu cha Kila siku halafu wanasema
wanataka watutoe hapa sasa tutaenda wap”? alisema Juma Masambo mfanyabiashra
katika Soko hilo
Akiongea kuhusu Malalamiko hayo
Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Vincent Nyerere alisema kuwa hakuna
Mfanyabiashara yeyote atakayeondolewa katika eneo la Soko la Mwigobero bila
kuonyeshwa sehemu nyingine ya kufanyia
biashara hiyo.
Akiongea kwa njia ya Simu kutoka Jijini
Dar es Salaam,Mh Nyerere alisema kuwa zipo taarifa kuwa Wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondoka katika
Eneo hilo la Soko la Mwigobero kupisha ujenzi wa soko la kisasa kwa ushirikiano
na Mamlaka ya Bandari.
Mh Nyerere katikati akitetea jambo na wabunge wenzake
Aidha aliongeza kuwa Wafanyabiashara
wote waliopo katika eneo hilo hawataondoka eneo hilo bila kupewa eneo
lingine,amesema Wafanyabiashara hao watapata Vibanda sehemu watakayotengewa
hivyo waondoe wasiwasi.
‘Yap ni kweli lakini mimi
nataka kusema kuwa hao wafanyabiashra wasiwe na wasiwasi maana hakuna
Mfanyabiashara atakayeondoka hapo bila kupewa eneo la kufanyia biashara”
alisema Mbunge huyo
Naye Mstahiki Meya wa Manisspaa yaa
Musoma Alex Kisurura akiongelea Sakata
hilo alisema kuwa tayari Mamlaka ya
Bandari imetoa fidia kwa wafanyabiashara 46 walikuwa ndani ya soko hilo wakati wa
Tathimini.
Kwasababu hiyo Mstahiki Meya alisema kuwa wananchi wa eneo hilo la
Mwigobero hawapaswi kuwa na hofu katika kufanyabiashara katika eneo hilo na
hivyo kuwataka wafanyebiashara zao kwa amani.
‘Mimi naweza kusema wafanyabiashara hao wasiwe
na wasiwasi kwani lazima tuhakikishe wanapata Maeneo mengine ya kufanyia
Biashara” alisema Mstahiki Meya
Eneo la soko la Mwigobero linatarajiwa kujengwa
kisasa kwa mujibu wa Viongozi hao ambapo Manispaa ya Musoma itashirikiana na
Mamlaka ya Bandari kufanikisha Ujenzi huo
No comments:
Post a Comment