POLISI WAUWA WAWILI NA KUJERUHI MMOJA
MGODI WA NOTH MARA.
Dinna
Maningo,Tarime.
WATU wawili
wamekufa na mwingine kujeruhiwa na askari polisi wanaolinda Mgodi wa Dhahabu wa North Mara
Nyamongo baada ya kudaiwa kuhusika na kuingia ndani ya mgodi kwa nia ya kupora
mawe yenye dhahabu.
Kamanda wa
polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo ambapo alisema kuwa watu wanaokadiriwa kuwa 800 maarufu kama
intruda wakiwa na silaha za jadi aina ya panga,Nyundo na Mawe walivamia maeneo
hayo kwa nia ya kupora dhahabu
Kamugisha
alisema kuwa mnamo agost 30 majira ya saa 12 jioni maeneo ya Rompad na shimo la
Gokona wakati polisi wakiwa kwenye jitihada
za kuwazuia na kuwaondoa intruda hao watu wawili waliuwawa baada ya kupigwa risasi
na polisi ambapo Paulo Sarya (26) mkazi
wa Nyangoto na Rodgers Mwita mkazi wa Kimusi waliuwawa huku Mseti Chacha
akijeruhiwa kwa kupigwa risasi
kwenye goti la mguu wa kulia na kulazwa hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Kamugisha
alisema kuwa askari mmoja No. E
6059 D/CPL Julius amejeruhiwa na maintuda kwa kukatwa panga usoni na kupata
majeraha mdomoni na mgongoni.
Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime Marco Nega alithibitisha kupokea mihili ya marehemu
wawili pamoja na majeruhi mmoja anae endelea
kupata matibabu hospitali ya Wilaya ambapo kwa upande wa Askari polisi alisema kuwa
hawana taarifa yoyote kuhusu askari polisi na hospitali yake haijampokea askari
yeyote.
“ Jana mida ya saa 2 usiku tumepokea mihili ya
marehemu wawili Lucas mwita Marwa (20) mkazi wa Kimusi tumemfanyia uchunguzi
alipigwa risasi karibu na shingo na kutokezea kifuani upande wa kulia na
kuharibu ubavu na mishipa kukatika na kusababisha kuvuja kwa damu nyingi na
kusababisha kufa” alisema Nega.
Aliongeza”
Mwingine ni Paulo Sarya (26) mkazi wa kijiji cha Matongo alipigwa risasi mguu
wa kulia karibu na goti na kutokezea kwenye paja na kusababisha kukatika kwa mshipa wa damu na
hivyo kuvuja damu nyingi na kusababisha kifo,Chacha Mseti(20) mkazi wa Nyamwaga
amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguu wa
kulia na yuko wodini anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri hao
ndio watu tuliopokea wote wamepigwa kwa risasi za moto nimekagua wodi zote
hakuna Askari polisi yeyote aliyepokelewa”alisema Nega.
Hata hivyo
Majeruhi Chacha Mseti aliliambia mwananchi
wodini hapo kuwa akiwa barabarani jirani na Mgodi wa
Gokona askari wakiwa wanawatawanya watu kwa risasi wanaodaiwa kuvamia mgodi
aliweza kushambuliwa na kisha kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.
No comments:
Post a Comment