ASKARI POLISI MMOJA MKOANI KIGOMA
AFARIKI KATIKA AJALI YA PIKIPIKI
Na Pardon Mbwate na Felister
Chubwa wa Jeshi la Polisi Kigoma
KIGOMA JUMATATU APRILI 30, 2012. Askari
Polisi mmoja wa Kikosi cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Kostebo
Shaban Hamisi Gobeka(37), amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokua
akiendesha kuacha njia na kugonga mti kushoto pembeni mwa barabara ya Lumumba mjini
Kigoma.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishns
Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa
12.15 jioni katika mtelemko mkali eneo la Lubengela wakati askari huyo akiendesha
pikipiki yenye namba T.757 BYY aina ya Toyo akitokea Mwanga kuelekea Kigoma
mjini.
Kamanda Kashai amesema wakati wa ajali hiyo
Kostebo Gobeka mwenye namba F. 1561 alikuwa amempakia kijana mwingine aitwaye Filbert
Kibuka(25) mkazi wa Mwanga mjini Kigoma ambaye yeye amejeruhuwa vibaya na amelazwa
katika Hospitali ya mkoa Maweni kwa matibabu zaidi na hali yake imeelezwa kuwa
ni mbaya.
Amesema ingawa Polisi bado inachunguza
chanzo cha ajali hiyo, lakini imebainika kuwa imesababishwa na mwendo kasi
uliotokana na kukatika kwa bleki ya pikipiki hiyo huku ikiwa kwenye mteremko
mkali.
Kamanda Kashai amesema Konstebo Gobeka alikuwa
ni dereva wa kutumainiwa wa pikipiki za Polisi na alipata mafunzo ya uendeshaji
wa pikipiki ambapo kabla ya kuhamishiwa kikosi cha mawasiliano ya Polisi mkoani
hapo, marehemu alikuwa ni miongoni mwa askari waliokuwa wakiendesha pikipiki za
doria mkoani Kigoma na hakuwa na kumbukumbu zozote za ajali.
Hata hivyo Kamanda
Kashai amesema Jeshi la Polisi limempoteza Askari shupavu na mchapakazi lakini
pia amesema pikipiki aliyopatanayo ajali Askari huyo haikuwa mali ya Jeshi la
Polisi.
No comments:
Post a Comment