WAJUMBE WA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA SADC WAANZA KUWASILI ZANZIBAR
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanziabr
ZANZIBAR
JUMAMOSI SEPTEMBA 1, 2012. Wajumbe wa Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya
Polisi kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SARPCCO)
wameanza kuwasili mjini Zanzibar tayari kwa kuhudhuria mkutano huo
utakaofanyika Septemba 5, mwaka huu.
Wajumbe
waliowasili leo ni pamoja na Mkuu wa INTERPOL. Kanda ya nchi za Kusini
mwa Afrika zilizopop Harare nchini Zimbabwe Bw. Chilika Simfukwe, pamoja
na maafisa wengine wa ofisi hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP
Mussa Ali Mussa, amesma mkutano huo utafunguliwa na Makam wa wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Gharib Bilali.
Awali
Mkutano huo ulitarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk.
Jakaya Kikwete ambaye atakuwa na shughuli nyingine za kitaifa.
Kamishna
Mussa amesema kuwa wengi wa wajumbe watakaowasili mjini Zanzibar ni
wale wa mikutano midogo midogo ya Kamati Tendaji za Wataalam wa vitengo
mbalimbali vya Majeshi ya Polisi kutoka nchi wanachama mikutano ambayo
itafanyika kuanzia Septemba 3 hadi 4, mwakahuu.
Amesema
kuwa mazimio yatakayofikiwa na kila kamati, yatafikishwa na
kuchambuliwa na Wakuu wa Majeshi ya Polisi katika mkutano wao wa
Septemba 5, mwaka huu.
Amesema
kuwa wakati wa mkutano huo, kutafanyika gwaride maalumu la kukabidhi
kitara kwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho hilo ambacho ni alama ya
uwenyekiti wa Shirikisho hilo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema,
anatarajiwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshio la
Polisi Afrika ya Kusini kamishna Jenerali Bi. Mangwashi Phiyega
anayemaliza muda wake.
No comments:
Post a Comment