Wednesday, August 8, 2012

 MADIWANI WA KATA 17  KATI YA 34 WAGOMA KUWA CHINI YA DC WA BUTIAMA


MUSOMA.

Madiwani wa kata 17  kutoka kambi ya upinzani na baadhi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Musoma, wamesema kamwe hawataunga Mkono kwa Madiwani hao kuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Butiama.

Wakiongea katika kikao cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Musoma,Baadhi ya madiwani wamesema kuwa wako tayari kuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Musoma na si Butiama kama baadhi ya viongozi wa Halmashauri hiyo wanavyotaka.

Wamesema kama wataruhusu suala hilo kupitishwa katika baadhi ya vikao,wananchi wa tarafa ya Nyanja watakuwa mbali na Makao makuu ya wilaya hiyo na hivyo kudai kuwa ni bora wakawa karibu katika wilaya ya Musoma.

Kuwepo kwa mvutano huo kutoka kwa madiwani wa kata 17 kati ya madiwani  wa kata 34 kunafuatia madiwani hao kudai kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw.Magina Magesa na Makamu Mwenyekiti  wa Halmashauri hiyo Bw. Denis Ikwabe kulazima kata hizo kuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Butiama.

Kufuatia mzozo huo na kutoelewana ndani ya kikao hicho Madiwani hao waliamua kutoka ndani ya Ukumbi huo na kukaa nje mpaka pale hoja nyingine ilipoendelea.

Miongoni mwa kata kumi na saba zinazopinga kuwepo chini ya mkuu wa Wilaya ya Butiama ni Pamoja na Kata ya Nyegine,Etaro,Nyakatende,Mugango,Kiriba,Suguti,Nyamrandirira,Nyambono,Bugwema,Murangi,Bukima,Bulinga,Bwasi,Makojo Bukumi,Tgeruka na Kata ya Busambara.

No comments:

Post a Comment