Thursday, June 7, 2012

                           JAMII YASHINDWA KUFUATA MISINGI YA HAKI ZA WATOTO

IMESEMEKANA KUWA JAMII IMESHINDWA KUFUATA MISINGI  YA HAKI ZA WATOTO NA KUPELEKEA WATOTO WENGI KATIKA JAMII KUKUA KATIKA MAADILI YASIYO SAHIHI.

HAYO YAMESEMWA NA MWEZESHAJI NA MRATIBU WA UMOJA WA MAENDELEO BUKWAYA (UMABU) BW. BULUDE NDAGO KATIKA WARSHA INAYOENDELEA KATIKA UKUMBI WA DAYOSISI YA ANGLIKANA MJINI MUSOMA

AMESEMA  NUSU YA WATANZANIA NI WATOTO HUKU ASILIMIA KUMI YA WATOTO HAO WAMEFIWA NA WAZAZI WAO,ASILIMIA 65 WANAISHI NA WAZAZI WOTE HUKU ASILIMIA 19 WAISHI NA MAMA ZAO PEKEE

BW. NDAGO AMESEMA ASILIMIA 5 YA WATOTO HAO HUISHI NA BABA ZAO HUKU ASILIMIA KUMI NA TISA YA WATOTO HAO WANAISHI BILA KUWA NA WAZAZI WALA WALEZI.

AMESEA KUNA NGUZO ZA HAKI ZA MTOTO AMBAZO NI PAMOJA NA HAKI YA KUISHI,HAKI YA KULINDWA,HAKI YA KUENDELEZWA,HAKI YA KUSHIRIKISHWA NA HAKI YA KUTOBAGULIWA.

AIDHA AMEONGEZA KUWA KUMEKUWEPO NA VITENDO AMBAVYO VINASABABISHA WATOTO WENGI KUISHI KATIKA MAZINGIRA AMBAYO SI RAFIKI KATIKA MAKUZI YA MTOTO.

AMETAJA VITENDO HIVYO KUWA NI PAMOJA NA UBAGUZI,UBAKAJI WA
WATOTO,MAUJI,KUTENGANA KWA WAZAZI,UNYANYASAJI,LUGHA MBAYA KWA WATOTO NA UGUMU WA MAISHA KATIKA FAMILIA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment