Thursday, June 7, 2012

              HALMASHAURI YAPANUA WIGO WA MAZINGIRA

Dinna Maningo,Tarime

HALIMASHAURI ya wilaya Tarime mkoani Mara imepanua wigo wa mazingira hadi mashuleni kwa kuhamasisha wanafunzi katika zoezi zima la  upandaji miti ilikufanya  sura ya nchi kuwa  katika hali ya kijani.

Zoezi la upandaji miti katika Halmashauri ya Tarime kwenye maadhimisho ya kilele ya sikukuu ya mazingira ambayo falinyikia  Eneo la Shule ya Sekondari Nkende kiwilaya wanafunzi pamoja na walimu wao walishirikishwa katika zoezi hilo.

Mgeni Rasimi wa maadhimisho hayo Diwani  Selvesta Marwa Kisyeri toka kata ya Komaswa ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime aliwataka wananchi kulinda na kutunza  mazingira kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijavyo.

Aidha Kisyeri aliongeza kuwa kuna haja kwa kila mwanchi kuwa mlinzi wa mazingira kwa kuyalinda na kuyatunza  na pia kuwa  mlinzi kwa yeyote anaye haribu mazingira ili kutoa taarifa panapo husika kuchukuliwa hatua za kisheria.

''Nitashirikiana na shule punde nitakapo hitajika katika swala zima la  maendeleo pia nitahakikisha kuwa mazingira ya shule yenu yanaboreshwa kwa kutumia nafasi niliyo nayo ngazi ya Halimashauri na pia kwa kutumia nafasi  hiyo nitaishawishi Halmashauri yangu kuwapatia miche ya miti 300 kwa jili ya kupanda shuleni kwenu  lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya sekondari hii ili iwe ya kwanza kwa mazingira bora  kiwilaya ''alisema Kisyeri.

Aidha Kisyeri alifafanua kuwa kulinda na kutunza mazingira ni swala la kila mmoja kutokana na kuwa kumekuwa na tatizo la kuchafua mazingira na kusababisha uchafuzi kama vile kukoswa hewa safi sanjari na vipato vyetu kudumaa kwa sababu ya  uharibifu wa mzaingira ambayo yanatokana na  kukata miti kuchoma mkaa,kuchoma Nyasi moto na kupanda miti isiyo rafiki katika vyanzo vya maji.
     
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment