VIONGOZI DIWANI CHADEMA TARIME WASWEKA MAABUSU
Na Shomari Binda
Tarime,
Viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wilayani Tarime pamoja na Diwani anayetokana na Chama hicho wamepelekwa
maabusu hii leo baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa
kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi na kufanya fujo katika chumba cha
kuhifadhia Maiti kaika hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Mbele ya
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime Yusto Ruboronga inadaiwa
June 5 mwaka huu washitakiwa hao wakiwa katika hospitali ya Wilaya ya
Tarime waliwazuia ngugu wa marehemu kuuchukua mwili wa ndugu yao naoa
maneno ya uchochezi wakidai kutaka kufanyiwa uchunguzi wa kina kabla
kuzikwa ili kujua sababu ya kifo cha Mogosi Chacha.
Washitakiwa
hao ambao ni Mwenyekiti wa Wilaya Lucas Ngoto,Katibu Mwita Mroni pamoja
na Diwani anayetokana na Chama hicho cha (CHADEMA) wa kata ya
Nyamisangura Christopher Chomete wanadaiwa kusababisha usumbufu katika
hospitali hiyo ya Wilaya ya Tarime huku wakitoa maneno ya uchocheze juu
ya tukio la kifo hicho cha Mogosi kilichotokea katika Mgodi wa Nyamongo.
Washitakiwa wote watatu wamekana mashitaka yao mara baada ya maelezo
kutoka katika pande zote za mashitaka na kupelekwa maabusu hadi June 16
baada ya kunyimwa dhamana kutokana na kuhofia kurudi katika eneo la
msiba kwenda kuendeleza kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya ndugu wa
marehemu.
Marehemu Mogosi Chacha aliuwawa kwa kupigwa risasi na
askari wa jeshi la Polisi June 4 baada ya kudaiwa kuvamia katika Mgodi
wa Nyamongo na kumjeruhi mlinzi wa mgodi huo Winchlaus Petro pamoja na
kutaka kumkata askari na panga ndipo alipopigwa risasi ya pembeni ya
mkono na kupitia ubavuni na kupelekea kifo chake.
kwa hisani ya BINDA NEWZ
No comments:
Post a Comment