MWANAFUNZI AFARIKI KWA BOM KIGOMA NA WENGINE WANNE WAJERUHIWA
Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi
Mwanafunzi
mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kigadye wilaya ya
Kasulu mkoani Kigoma, Abeid Manase(8), amefariki dunia hapo hapo na
wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa
kwa mkono walilokuwa wakilichezea.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja watoto
waliojeruhiwa na bomu hilo kuwa ni wanafunzi wawili wa darasa la kwanza Tuju Seluke(7) aliyejeruhiwa tumboni na Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa kwenye paja na mguu kulia. wote wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kigadye wilayani Kasulu.
Kamanda
huyo amewata wengine waliojeruhiwa kuwa ni watoto wadogo wenye umri wa
miaka minne kila mmoja ambao walikuwa wakichezea bomu hilo kwa pamoja
ambao ni Enjord Seluke aliyejeruhiwa kwenye sikio la upande wa kushoto na Isaka Yohana aliyejeruhiwa kwenye jicho la upande wa kushoto.
Kamanda
Kashai amesema majeruhi hao wote wamelazwa katika hospitali ya Misheni
iliyopo katika kijiji cha Shunge wilauani Kasulu kwa matibabu zaidi na
hali zao zimeelezwa kuwa zinaendelea vizuri.
Kamanda
Kashai amesema jana majira ya saa 11.00 jioni, huko katika kijiji cha
Kigadye, watoto hao walikuwa wakilichezea bomu hilo la kutupa kwa mkono
na ndipo lilipowalipukia na kumuua mwenzao na wengine hao wane
wakajeruhiwa.
Bomu hilo lilikuwa limefichwa katika moja ya bustani nyumbani kwa Bw. Ayoub James Luvahovi mkazi wa kijiji cha Kidae na likimbia mara baada ya tukio hilo na Polisi wanamsaka.
Katika
tukio linguine Kamanda Kashai amesema huko Kasulu, watu wenye silaha
wamemjeruhi kwa kumpiga risasi tumboni mfanyabiashara mmoja Bi. Deothera
Malusha(23) na baadaye kumpora shilingi 150,000 pamoja na simu yake ya
mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 55,000.
Amesema
baada ya uporaji huwo, majambazi hayo yalikimbia na kutokomea katika
msituni na majeruhi amelazwa kwenye Hospitali ya wilaya ya kasulu mkoni
Kigoma na hali yake bado sio nzuri.
Wakati
huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhamiaji
haramu 52 kwa makosa ya kuingia na kuishi nchini bila ya kibali.
Kamanda
Kashai amesema kuwa wayuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali
walipokuwa wakifanya shughuli za uvuvi mkoani humo.
Mwisho
SOMO LA POLISI LA USALAMA WETU KWANZA LAINGIZWA KATIKA MTAALA WA SHULE ZA MSINGI ZANZIBAR.
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, leo imezindua rasmi somo la Polisi la litakalojulikana kama Usalama wetu kwanza kuwa moja ya masomo yatakayofundishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi visiwani humo.
Akizungua
mpango huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mh. Ali
Juma Shamhuna, amesema kuwa somo hilo litaanza kufundishwa kwa majaribio
katika shule kumi za msingi kisiwani Unguja na hivyo kulifanya somo
hilo kuwa sehemu ya masomo yaliyopo katika mitaala ya shule za msingi
Visiwani hapa.
Mh.
Shamhuna amesema kuingizwa kwa somo hilo katika mitaala ya shule za
msingi, kutasaidia kujenga uwezo na uwelewa wa kujitambua na katika
kuwabaini wahalifu mbalimbali wakiwemo maadui wa taifa letu.
Mh.
Shamhuna ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mpango huo,
amekagua vitabu vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo ambavyo
vimeandaliwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kwa ajili hiyo.
Awali
katika Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani hapa Bi.
Mwanaidi Salehe Abdallah, alisema kuwa somo la Usalama wetu kwanza
litakuwa kama somo linguine na litatungia mitihani ya kujipima na ule wa
Taifa.
Somo
la Usalama wetu kwanzxa ni somo lililobuniwa na Jeshi la Polisi hapa
nchini ili kuwawezesha wananfunzi wa shule za msingi na sekondari
kujenga uwelewa katika matumizi salama ya usalama barabara kwa lengo la
kuepuka ajali za mara kwa mara.
Naye
Mwakilishi wa Kamishna wa Polisi zanzibar ACP Mohammed Ali Mweri,
amesema kuwa somo la Usalama wetu kwamza limeanzishwa na jeshi la Polisi
na ni moja ya Miradi ya Polisi Jamii inayomjenga mtoto katika
kuwatambua watu wabaya na jinsi ya kuwaepuka na hata kuwatolea taarifa
katika vituo vuya Polisi.
Wakati huo huo,
Mh. Shamhuna amekemea vikali baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu
kutaka kuhatarisha usalama wa Taifa letu kwa kudai kura ya maoni juu ya
Muungano kabla ya shughuli za ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya Jamhuri
kukamili.
Amesema
watu hao ni hatari kwa Taifa letu na kwamba Serikali haiwezi kukaa
kimya kuona amani inavurugika kutokana na kikundi cha watu wachache kwa
imani za itikadi ya kidini.
Amesema
tangu kukusanywa kwa maoni yaliyoandika Katiba mpya ya Zanzibar yenye
sura ya Umoja wa Kitaifa, hivi sasa Zanzibar vimekuwa tulivu na eneo la
mfano kwa nchi za Kiafrika zenye utulivu.
Amewataka
Watanzania kuwaepuka na kuwabeza wale wote wenye kuleta migogoro na
kutaka kuiingiza nchi yetu katika vurugu zisizo na msingi na badala yake
kila mmoja awe mtulivu na kujishughulisha na kazi zinazoleta maendeleo.
Wakati
wa risala yao, wanafunzi kutoka shule kumi zitakazofundisha kwa
majaribio somo la Polisi la Usalama wetu kwanza, wameiomba Serikali
kutowafumbia macho wale wote wanaochochea vurugu na ghasia kwani
wamesema yanapotokea machafuko, wanaoathirika zaidi ni wale wasiojiweza
wakiwemo walemavu, wazee, wanawake na watoto.
Naye
mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi darajani Rashidi Ali
Mohammed, amesema kuwa somo hilo litawapa wanafunzi ujasiri wa kuweza
kutoa taarifa Polisi pale wanapoona vitendo vya uhalifu mbele ya macho
yao.
ujasiri
kapoa Polisi litamwanafunzi Shule kumi za msingi zitakazoanza kunufaika
na Somo hilo la Polisi ni Darajani, Makadara, Migombani, Chumbwini,
Muungano, Shaurimoyo, kilimahewa “A”, Rahaleo, Jang’ombe na Mkunazini
zote za mjini Zanzibar.
Mwisho
No comments:
Post a Comment