MISITU YA ASILI KUTOWEKA KAGERA
Na Ashura Jumapili,Bukoba,
IMEELEZWA kuwa hali ya misitu mkoani Kagera hairidhishi
kutokana na kasi ya kutoweka kwa misitu ya asili katika maeneo yaliyohifadhiwa
na yasiyohifadhiwa iliongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo zaidi ya
hekta 68,508 ambazo hazijahifadhiwa kisheria.
Hayo yameelezwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa ( RCC )na Jafar Omar
kutoka ofisi ya maliasili Mkoa wa Kagera, wakati akitoa taarifa ya katika kikao hicho ya kupandishwa hadhi kwa hifadhi yam
situ wa Taifa,Minziro kuwa Hifadhi Asilia.
Omar alisema hali ya misitu kutoridhisha mkoani Kagera
kunachangiwa na kutokuwa na
mipaka inayotambuliwa,kutokuwa na mpango wa usimamizi hadi 2011ni msitu mmoja
tu ndio una mpango wa usimamizi pamoja na uvunaji holela wa miti na uvamizi wa
maeneo yam situ.
Alisema sababu nyingine ni uchungaji haramu wa mifugo katika
hifadhi za misitu na mapori ya akiba,ujenzi holela wa makazi katika hifadhi za
misitu,uchimbaji wa madini ndani ya
hifadhi,kilimo cha mazao mbalimbali ndani ya hifadhi na ukataji miti ovyo kwa
ajili ya uchomaji mkaa.
Alisema visababishi vya uharibifu wa misitu ni ongezeko kubwa la watu( ndani na nje ya mkoa ),uhaba
wa ardhi yenye rutuba,kupanda kwa gharama ya nishati mbadala kama vile umeme na
gesi.kupanda kwa gharama ya malighafi mbadala katika ujenzi wa nyumba na makazi.
Aliongeza kuwa uwezo mdogo wa sekta ya misitu katika
kusimamia Rasilimali hiyo,upungufu wa fedha na watumishi.
Hata hivyo alisema mikakati ya kuokoa misitu hiyo inaendelea
ikiwa ni pamoja na mamlaka ya za serikali za mitaa zinaendelea kutekeleza
sheria ndogo zilizowekwa kulingana na mazingira ya eneo husika.
Alisema sheria zimepitishwa kwa mifugo yeyote inayoingia
katika mashamba ya miti ya watu au taasisi kutumiwa kama kitoweo cha taasisi au
mmiliki wa shamba husika.
Aidha alisema sheria hiyo imesaidia katika utunzaji wa miti
na misitu ya kupanda katika halmashauri ya Wilaya ya Chato.
No comments:
Post a Comment