Wednesday, August 8, 2012

BABA ASKOFU ALIASA JESHI LA POLISI TARIME.

DINNA MANINGO,Tarime

BABA Askofu wa Kanisa la Anglicana Dayosisi ya Tarime Mwita Akili amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kujenga mahusiano mazuri na jamii kupitia polisi jamii ili wananchi wawe na imani na jeshi hilo.

Askofu Mwita Akili ameyasema hayo leo katika ofisi ya Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya  wakati akikabidhi mipira 25 kwa kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha kwa ajili ya mashindano  yanayoendelea ya  Polisi jamii Kata Cup 2012 katika Mkoa huo wa kipolisi yenye lengo la kujenga uhusiano baina ya polisi na wananchi .

 Askofu Akili amesema kuwa endapo jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Tarime /Rorya litafanya  kazi kwa kufuata maadili  pamoja na kutenda haki ni hakika wananchi watakuwa na imani na jeshi la polisi na kwamba kusipokuwa na mahusiano mema jeshi hilo litakosa taarifa muhimu kutoka kwa raia hususani  katika kuwafichua waharifu


Hata hivyo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema kuwa jeshi la Polisi limeanzisha program za mafunzo  mara 2 kwa wiki  kwa polisi lengo likiwa kuwataka polisi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili pamoja na kutenda haki.

No comments:

Post a Comment