Monday, August 13, 2012

NAULI MPYA YAWASOTESHA ABIRIA STENDI.

Dinna Maningo,Tarime.

ABIRIA  waliokuwa wakisafiri kwenda maeneo mbalimbali Wilayani Tarime na Musoma Mkoani Mara wameshidwa kusafiri na kisha kuendelea kusota stendi baada ya wamiliki wa magari kugoma  kusafirisha Abiria baada ya Sumatra kushusha viwango vya nauli ambapo polisi wanafanya zoezi la kukagua tiketi kwa abilia wanaosafiri.

 Kwa mujibu wa maelezo ya wamiliki wa magari Tarime walisema kuwa Viwango vipya vilivyopangwa na Sumatra Kutoka Wilayani Tarime hadi Musoma ni 2900  mwendo wa km 87ambapo kwa nauli ya zamani ilikuwa sh 4,000, magari yatokayo Tarime kwenda Shirati ni 1,700 bei ya zamani 5,000 km 57,magari yatokayo Tarime kwenda Nyamongo 1,700 km37 bei ya zamani 5,000,magari yatokayo Tarime kwenda Sirari  700 km18 bei ya zamani ilikuwa 1,500,Tarime hadi Mugumu 5,800 bei ya zamani 7,000.

Baadhi ya wamiliki wa magari walisema kuwa viwango vya nauli  vilivyopangwa na mamlaka ya usafirishaji SUMATRA  ni vya chini mno na nihasara kwao kutokana na kiwango kikubwa cha mafuta kilichopo pamoja na gharama kubwa za vifaa na matengenezo.

Hivyo wameitaka SUMATRA kurekebisha viwango hivyo na kuwa mgomo huo ni endelevu hadi pale Serikali itakapo sikiliza vilio vyao  nakufanya mabadiliko ya bei hiyo mpya ya nauli kwa wasafiri.

Devid Mkunyi alisema kuwa maamuzi hayo ya viwango vipya yanajenga taswira mbaya kwa wafanya biashara kwa madai kuwa bei iliyotolewa imepitwa na wakati kwani haiangalii mazingira ya usafirishaji hususani barabara itokayo Tarime-Nyamongo ambayo si ya Rami

 Kutokana namugomo huo  wa wamiliki wa magari  baadhi ya abiria walisema kuwa kitendo cha magari kutofanya safari zake  kimewaathiri baada ya kustisha safari kwa shuguli zao mbalimbali nakwamba mgomo huo wa wamiliki umesababisha  watu kusafiri Kutoka Wilayani Tarime kwa usafiri wa  kukodi kwa nauli sh elfu hadi 50,00 kwenda Musoma tofauti na nauli ya zamani ya Sh 4,000,


Hata hivyo Ofisa Mfawidhi Mamlaka ya usafirishaji Sumatra Mkoa wa Mara Maico Lojasi alisema kuwa viwango vilivyopamgwa vimefuata talatibu zote za usafirishaji na kiuchumi na kwamba wamiliki wa magari wamekuwa wakijipangia nauli zao wenyewe jambo ambalo linaathiri abiria.

No comments:

Post a Comment