SERIKALI NA VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUSHIRIKIANA
Arusha,-
Serikali za Afrika Mashariki na vyombo vya habari
zinatakiwa kufanyakazi kama wadau, huku zikihakikisha kuendelea kuwapo kwa uhuru
kwa kila upande katika utendaji wa majukumu yao.
Waandishi hao
walitoa tamko hilo katika mkutano wa tano wa Vyombo ya Habari vya Afrika
Mashariki ulionfanyika mjini Kigali, Rwanda ambapo pia waliwaomba wamiliki wa
vyombo hivyo kutoa fursa za mafunzo kwa waandishi wao kuwawezesha kujiimarisha
taaluma ili kuandika ipasavyo habari katika nchi tano wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC).
“…Tunataka
vyombo vyetu vya habari kutoa habari za EAC kutoka kwenye muonekano wa EAC;kwa
kuzingatia ukweli wetu badala ya kuegemea vyanzo vya habari za nje ambavyo
vinaweza kuwa kinyume na malengo ya EAC,” yanasomeka maazimio yaliyotolewa
mwishoni mwa mkutano huo wa siku mbili ambapo Shirika huru la Habari la Afrika
Mashariki (EANA) lilibahatika kupata nakala zake.
Katika maazimio
hayo ya vyombo vya habari Afrika Mashariki, hasa wahariri, wanatakiwa kuvipa
kipaumbeke habari zinazoihusu EAC kwa kuvipa nafasi na muda unaohitajika kwenye
vyombo vyao wanavyoviongoza.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Katibu Mkuu wa EAC ,Dk Richard
Sezibera, Spika wa Bunge la EAC, Margret Zziwa, na mameneja wa vyombo vya
habari, pamoja na wengine katika ukanda huo.
Pia mkutano huo
uliwasihi wamiliki wa vyombo vya habari kubuni ushindani wa ndani utakaoibua
majadiliano katika maswala mbalimbali juu ya jumuiya kushawishi uelewa kuhusu
mtangamano wa EAC kwa upana.
‘’Mameneja wa
vyombo vya habari wanawajibu wa kufuatilia na inapobidi kusimamia utoaji wa
habari kwa kiwango kinachohitajika, ikiwemo ubora na usahihi,’’ walieleza.
Katika mkutano
huo, waandishi hao na Rais Kagame walijadiliana namna ya kuanzia uhusiano baina
ya vyombo vya habari na serikali ambapo Rais huyo aliwaambia waandishi hao
“kusema habari zetu” badala ya kuviachia vyombo vya habari vya magharibi ambavyo
mara kwa mara hupotosha ukweli.
Mkutano huo kwa
pamoja uliamua kuanzisha Baraza la Habari la Afrika Mashariki kama chombo cha
juu kitakachokuwa kinaratibu matumizi ya sheria na kanuni za habari katika
EAC.
Katika kuhabarisha juu ya maswala ya
jumuiya, Mkutano ulitoa changamoto kwa vyombo vya habari kuachana na matukio ya
EAC na kubaini fursa na changamoto zitakazowanufaisha wakazi ndani ya
jumuiya.
“Wakati
mnafurahia uhuru wa habari, waandishi mnatakiwa kuongozwa na taaluma, usahihi na
ulinganishi bila kuingilia haki za wasikilizaji wenu katika kupitisha
maamuzi.”
No comments:
Post a Comment