Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mwanafunzi wa
Darasa la Saba shule ya msingi Hogolo, aliyefahamika kwa jina la Matha Mazoea Mwenye umri wa Miaka (14) ameuawa kwa kunyongwa na kufukiwa kwenye
shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Akizungumzia tukio
hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen alisema tukio hilo
limetokea mnamo tarehe 11/08/2012 majira ya saa 08:00 asubuhi katika mtaa wa
Ikulu Kijiji cha Hogolo Kata ya Hogolo tarafa ya Zoisa Wilaya ya Kongwa.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha
mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani marehemu alikuwa amevunja uhusiano na
mpenzi wake wa muda mrefu aliyejulikana kwa jina la Heri Aboubakar na kuanzisha
uhusiano na mpenzi wake mpya aliyefahamika kwa jina la Wilfredy Muhaha @ Kabo mwenye
miaka (17) “ Alielezea Kamanda Zelothe
Katika tukio hilo Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji hayo
ambao ni Asha Jafari Mohamed mwenye umri wa miaka 16, mkulima, mkazi wa Mtaa wa
Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea mwenye umri wa miaka
21, Mkulima, Mkazi wa Ikulu Hogolo Wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Bw.
Zelothe alieleza kwamba ili kufanikisha
uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi pia Wilayani humo linamshikilia mpenzi mpya wa marehemu Bw. Wilfredy s/o Muhaha pamoja na kumtafuta mpenzi wa zamani wa marehemu Bw. Heri s/o Aboubakar ambaye amekimbia
kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa.
Aidha kamanda Zelothe
alisema Katika tukio hilo Kaka wa marehemu ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi, katika
maelezo yake ya awali alidai kusikia
purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakuweza
kutoka usiku huo ili kushuhudia nini kinaendelea.
Kamanda Zelothe
alisema Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo Kijijini na kwamba
siku ya tukio walikuwa wameondoka kwenda katika Vijiji vya jirani, ambapo bibi
yake na marehemu alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu
yake alikwenda kijiji cha Banyi banyi
kwa Shughuli za kutemebelea wagonjwa.
Wakati huo huo Gari
lenye namba za usajili T. 750 AEU aina ya TOYOTA CHASER likiendeshwa na Kenedy
James mwenye umri wa miaka 48, Mkazi wa Mpwapwa liliacha njia na kupinduka na
kusababisha kifo cha Salum Kaduma mwenye umri wa miaka (13) Mwanafunzi wa kidato
cha kwanza Katika shule ye sekondari ya Mpwapwa, na kusababisha kifo chake.
Mkuu huyo wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma alisema ajali hiyo ilitokea mnamo tarehe 12/08/2012
majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Kisima Wilaya ya Mpwapwa Mkoani
Dodoma.
“Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa magurudumu mawili ya
upande wa kulia kitu kilichopelekea gari hilo kuacha njia na kupinduka.” Aliongeza
Bw. Zelothe
No comments:
Post a Comment