Wananchi mkoani Mara wamepewa tahadhari juu ya Ugonjwa
wa Ebola ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepokea taarifa kutoka
shirika la afya Duniani WHO kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola ambao
umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda.
Mratibu wa Elimu ya afya na Malaria mkoani Mara Bi.
Tukae Lisso,amesema maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni kanda ya magharibi ya
nchi hiyo ya Uganda ambapo mpaka jana takriban watu 36 wamepata maambukizo na
kati ya hao 19 wamepoteza maisha.
Amesema kutokana na taarifa hizo kutoka nchi jirani
Wizara ya Afya na ustawi wa jamii nchini imetoa tahadhari kwa wananchi waliopo mikoa inayopakana na
nchi jirani ya Uganda kuwa Makini na ugonjwa huo.
Bi Tukae Lisso ametaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na mkoa
wa Mara,Mwanza,Kagera,Kigoma na Rukwa ambapo wananchi katika mikoa hiyo
wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa kutokana na ugonjwa huu wa Ebola.
Amesema dalili za ugonjwa wa Ebola ni pamoja na homa kali ya ghafla,kulegea mwili,Maumivu ya
Misuli,Kuumwa Kichwa na vidonda kooni,Bi Lisso ameongeza kuwa wakti mwingine
dalili hizo hufuatiwa na kutapika,kuharisha,vipele vya ngozi huku figo na in
hushindwa kufanywa kazi.
Kufuatia hatua hiyo Bi Lisso amesema ugonjwa wa
Ebola hauna tiba wala chanjo na hivyo amewataka wananchi mkoani Mara kuchukua
tahadhari wanapomuona mtu ambaye ana dalili za ugonjwa huo wa Ebola
No comments:
Post a Comment