MWANAFUNZI
WA KIDATO CHA PILI AFA KWA KUCHOMWA KISU.
Dinna
Maningo,Tarime
MSICHANA mmoja
Angelina Masero (18) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya
sekondari Nyawaga,mkazi wa kijiji cha Keisangura amekufa baada ya kuchomwa kisu
sehemu mbalimbali za tumbo na mwanafunzi mwenzie kutokana na sababu za wivu wa
kimapenzi.
Akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwakwe Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi
Tarime/Rorya Justus Kamugisha alisema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 30
julai 2012 majira ya saa 5 asubuhi nakwamba mwanafunzi aliyehusika na tukio hilo ni Muhono Manko
(22) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo hiyo ya Sekondari Nyamwaga ambaye ni mkazi wa
Nyamwaga.
“Baada ya
tukio hilo marehemu alipelekwa katika
hospitali ya Wilaya ya Tarime na kulazwa bahati mbaya jana siku hiyo hiyo
saa 5 usiku alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu chanzo cha tukio
kinasemekana kuwa ni wavu wa kimapenzi”Alisema Kamugisha
Kamugisha
alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kutenda kosa hilo alikunywa sumu
inayosadikiwa kuwa ni dawa ya kuoshea
mifugo kwa lengo la kutaka kujiuwa na
kujisalimisha kituo cha polisi Nyamwaga.
Alisema kuwa
mtuhumiwa ametibiwa katika kituo cha
afya Nyamwaga na kururusiwa na kwamba yuko kituo cha polisi Nyawaga kwa
mahojiano na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Wakati huo huo,
MTU mmoja
aitwae Sadec Stiven 17 mkazi wa Mika Wilayani Rorya Mkoani Mara amefariki dunia
baada ya mwili wake kukutwa ukielea majini ziwa Victoria
Kamugisha
alisema kuwa marehemu alikwenda kwa
ndugu zake waishio Bukwe kata ya Bukwe Wilayani Rorya siku ya tarehe 30 julai nakwamba
marehemu aliondoka bila kuaga hali ambayo iliwaladhimu ndugu kumtafuta.
Kamugisha
alisema kuwa mwili wa marehemu umepatikana leo majira ya saa 3 ukielea
majini nakwamba mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa wazazi
kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment