MWALIMU
MBALONI KWA KUDAIWA KUCHOCHEA WANAFUNZI KUANDAMANA.
Maximilliani Ngesi,Tarime
JESHI la Polisi
Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya
linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya Msingi Rebu Kata ya Turwa Wilayani
Tarime, Ester Kasika (40) kwa mahojiano baada ya kudaiwa kuhusika kuchochea watoto kufanya maandamano
baada ya kutokea kwa mgomo wa walimu hapo jana.
Akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi
Tarime/Rorya Justaus Kamugisha amesema kuwa kutokana na mgomo uliofanyika
jana, wanafunzi wa shule ya msingi Rebu
waliandamana kwenda ofisi Mkuu wa Wilaya Tarime kudai haki zao za kusoma.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Tarime/Rorya Justus Kamugisha
Kamanda wa Kanda Maalum ya Tarime/Rorya Justus Kamugisha
Kamugisha
amesema kuwa katika kufatilia mgomo wa walimu uliotokea jana imebainika kuwa
wanafunzi wapatao 50-60 wa shule ya msingi Rebu iliyopo Mjini Tarime waliamua
kufanya maandamano kuelekea ofisi ya Mkuu wa Wilaya Tarime kwa kile walichoelezwa kuwa wanadai
haki yao ya kusoma waliyoikosa kutokana na na mgomo huo wa walimu ambao unaoendelea
hadi hivi sasa wilayani Hapa.
Pia Kamugisha amewaonya baadhi ya walimu kuwatumia watoto kudai haki
zao nakuwa kitendo hicho ni kuvunja haki za watoto na kuwa Jeshi la polisi
halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kujihusisha
na vitendo vyovyote vya kuvunja sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment