Na Waitara Meng’anyi, Tarime.
Mwalimu wa shule msingi amekufa kifo cha mashaka akiwa katika starehe zake na mwanamke anayeaminika kuwa ni mpenzi wake bila kujulikana makazi yake katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Kwa mujibu wa Kamishina Msaidizi wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya APC Justus Kamgisha alimtaja kuwa ni Kaimu Yeremia (27) anayefundisha katika ya msingi Kegonga Wilayani humu.
“Marehemu alienda kwa mwalimu menzake aitwaye Focus Aloyce (33) aliyempa chumba akiwa na rafiki yake wa kike ambaye hajulikani jina wala makazi yake alasiri, lakini Aloyce aliporudi alimkuta marehemu ameanguka sakafuni akiwa na michubuko midogomidogo na jeraha dogo mdomoni akitokwa na mapovu mdomoni” ilisema APC Kamugisha.
Na kuongeza kuwa “ wakati huo mwanamke aliyekuwanaye akiwa hayupo na kuelekea kusikojulikana”.
Katika juhudi za kutaka kunusuru maisha yake marehemu alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibu hadi alipofariki dunia muda mfupi baadaye
Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya kifo hicho na huku likiendelea kumtafuta mwanamke aliyekuwa na marehemu kabla ya kifo chake kulingana na ACP Kamugisha.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda wilaya ya Bunda kwa maandalizi ya mazishi kulingana na uongozi wa idara ya elimu Wilayani Tarime.
Wakati huo huo watu wawili wameuwawa na watu wasiofahamika katika matukio tofauti tofauti Wilayani Tarime na katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Katika tukio la kwanza mkulima wa kijiji cha Nyabikondo Igina Kakoyo (38) aliuwa na watu wasiojulikana kwa kupigwa kwa fimbo na kitu kizito katika sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyompelekea kufariki dunia.
“ Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyealiyekamatwa kutokana na tukio hilo” ACP Kamugisha lisema.
Katika tukio la pili fundi ujenzi Seifu Makenge (39) mkazi wea kijiji cha Rebu Tarime aliuwawa katika kijiji cha Keisangura kwa kuchomwa kwa kisu tumboni na Marwa Baikuni.
“ Majeruhi alikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibabu na baada ya saa chache alipoteza maisha” alisema ACP Kamugisha.
Kwa mujibu wa ACP kamugisha chanzo cha kifo cha Makenge ni ugomvi uliotokea baada ya marehemu kudai shilingi 10,000/- alizokuwa akimdai mtuhumiwa.
Baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo alitorokea kusikojulikana na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta ili kumfikisha mbele ya sheria kujibu tuhuma zinzomkabili.
Kutokana vitendo hivyo vinavyozidi kuongezeka katika mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya jeshi la poli linatoa wito kwa jamii kutoa taarifa mapema kwa jeshi hilo mara tatizo linapotokea.
No comments:
Post a Comment