Bukoba,
JAMII ya Kitanzania imeshauriwa kuwa na mwamko wa kujifunza lugha ya alama ili kuwepo kwa mawasiliano mazuri katika huduma mbalimbali kwa watoa huduma na jamii ya viziwi.
Wito huo ulitolewa na mratibu wa mradi wa mafunzo ya alama kwa watoa huduma mbalimbali wa chama cha viziwi Tanzania ( CHAVITA) Ayoub Isack tawi la Mkoa wa Kagera katika warsha ya mafunzo hayo inayofanyika kwa muda wa siku nne katika Manispaa ya Bukoba .
Isack alisema kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa mafunzo ya lugha ya alama kwa wadau mbalimbali na wato huduma kwa jamii kama vile jeshi la polisi,mahakama,Banki, hosipatali, walimu pamoja na watu binafsi ili waweze kuelewa jinsi ya kutumia mawasiliano ya lugha hiyo ya alama ili waweze kupunguza vikwazo vya mawasiliano kati ya wanaosikia na jamii ya viziwi.
Mratibu huyo alisema kabla ya lugha ya alama hapakuwepo na mawasiliano mazuri yanayoeleweka kwa mfano kiziwi anapokwenda kupata huduma katika kituo chochote cha Afya au hata hospitali ilikuwa ni vigumu kuwasiliana na daktari ili aweze kupata matibabu.
Hata hivyo alifafanua kuwa kiziwi ni mtu aliyepoteza uwezo wa kusikia na hali hiyo inatokana na mtu huyo kuzaliwa akiwa kiziwi na wakati mwingine hutokea baada ya kuugua.
Aliongeza kuwa kitendo cha kumuita kiziwi kuwa ni mtu asiyesikia ni udharirishaji huku akifafanua kuwa mtu asiyesikia ni mkaidi na siyo kiziwi kwani kiziwi hutumia alama ya ishara na alama hizo siyo kwa viziwi tu bali kwa jamii nzima hata wanaosikia wakati mwingine hutumia alama fulani kuwasiliana.
Aidha alisikitishwa na jamii ya Tanzania ambayo imekuwa na tabia ya kumuunganisha bubu na kiziwi jambo ambalo sio sahihi huku kuwatofautisha mabubu na viziwi kwa madai kuwa bubu kuitwa kiziwi pia ni udharirishaji kwani bubu anasikia lakini hana uwezo wa kuongea na kiziwi hasiki lakini huongea kwa ishara.
mwisho
No comments:
Post a Comment