Na Dinna Maningo,Tarime
MTENDAJI wa kata ya matongo,Nyamongo Wilayani Tarime mkoani Mara BW. Deodatus Nyamuhanga Weikama amekamatwa kwa agizo la Mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele kwa madai kuwa mtendaji huyo amekuwa hatendei haki kwa wananchi.
Kukamatwa kwa mtendaji huyo kumekuja baada ya malalamiko ya wananchi kudai kuporwa ardhi yao na wanapopeleka malalamiko yao kwa mtedaji huyo hayatatuliwi badala yake mtendaji huyo amekuwa akisaidia kupora ardhi kwa kushirikiana na watuhumiwa.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kukamatwa kwa mtendaji huyo ni baada ya malalamiko ya Bi Nchagwa Kisire(36) kudai kuporwa ardhi na mme wake na kisha mme huyo na mtendaji kufunga mji wake kwa kufuri tangu tarehe 23 na kusababisha mama na watoto kuendelea kuishi kwa kuhifadhiwa na majirani.
“Nimeagiza akamatwe ili tumuhoji kwa sababu amekuwa akilalamikiwa na wananchi kutowatendea haki hasa katika utatuzi wa migogoro ya ardhi,mfano mama huyu alilalamika kunyang’anywa ardhi na mme wake ambaye alimtelekeza mkewe Nchangwa tangu mwaka 2001 na sasa anamyanga’a makazi yake mtendaji badala ya kutatua mgogoro yeye anashirikli kusaidia kunyang’anya ardhi!
Anaongeza’ Mtendaji aliitwa ili aje atoe majibu lakini hakufika ofisini na badala yake akapotea akuonekana hata kazini kwa muda wa wiki mbili na baada ya kusikia tetesi karudi nilikwenda Ofisini kwake nikaagiza polisi wamkamate ili aje atueleze na sasa tumemkamata yuko hapa ofisini kwa mahojiano zaidi”anasema Henjewele.
Mtendaji huyo amedaiwa kuwa amekuwa akishindwa kutatuwa migogoro ya wananchi na badala yake amekuwa akitumia nafasi ya cheo chake kuwanyanyasa wananchi.
Hata hivyo Mwandishi wa habari hizi aliwasiliana na mlalamikaji Nchagwa kisire ambapo alidai kuwa mnamo tarehe 23 mme wake alifika nyumbani kwakwe na kumtaka aondoke ambapo pia mmewe na mtendaji walifunga nyumba kwa kufuri hali ambayo imesababisha aendelee kuhifadhiwa na majirani.
Bi Kisire alisema kuwa chanzo cha mmewe kumnyang’anya eneo analoishi ni baada ya mama huyo kutalajiwa kuhamishwa na kampuni ya mgodi wa North mara Barrick baada yakuwa eneo analoishi liko jirani na mgodi wa North Mara
“Mme wangu alinitelekeza tangu mwaka 2001 mimi ni mke wa tatu na kila mwanamke alimpatia eneo lake la kuishi lakini baada ya eneo ninaloishi kutarajiwa kulipwa na mgodi mme kaja kapora ardhi yangu na kuniambia niondoke,nitaenda wapi na nina watoto 3chakushangaza toka anitelekeze hakuwai kunipa matumizi hata nyumba ninayoishi nimeijenga kwa nguvu zangu haki iko wapi? Ilinibidi niende ofisi ya Dc nikampelekea kilio change “anasema Nchagwa.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Jastus Kamugisha alisema kuwa walimkamata mtendaji huyo baada ya kuagizwa na mkuu wa wilaya Henjewele kwa madai kuwa amekuwa atendei wananchi haki hivyo anatakiwa kwenda kuhojiwa.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MWISHO,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment