Na Waitara Menganyi, Tarime.
WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi walivamia na kuua kwa kutumia silaha mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ntagacha Wilayani Tarime mkoa wa Mara.
Kwa mujibu wa kamishina msaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime/Rorya ACP Justus Kamugisha aliyeuawa alitajwa kuwa ni Masanju Mwita (70) mkazi wa kitongoji cha Nyankaria katika kijiji cha Ntagacha.
“Masanju alifariki dunia muda mfupi baada ya kupigwa risasi na kundi la watu wapatao 10 wakati akifuata nyanyo za wizi huo wa ng’ombe hao watatu” alisema RPC Kamugisha.
Kamugisha alisema kuwa usiku wa kuamkia juzi majira ya saa 5.30 watu walivamia kwa Joseph Mwita (38) na kupora ng’ombe watatu.
“Inadhaniwa kuwa majambazi hayo yalikuwa kumi na kutokana na risasi zilizo pigwa walitumia silaha ya AK 47” alisema kamanda wa polisi kanda maalumu ya ACP Kamugisha.
Ntagacha ulikuwa uwanja wa vita ya koo mbili za Wairegi na Wanyabasi ambapo vita hiyo ilikuwa ikisababishwa na wizi wa mifugo huku lawama zikirushiwa kila koo kuwa ndiyo anzilishi wa vita na wizi.
Kutokana na mauaji hayo jeshi la polisi Tarime/Rorya linaendelea na uchunguzi ili kubaini waharifu hao na kuwafikisha katika mbele ya sheria.
“Msako mkali unaendelea wa jeshi la polisi la Tarime/Rorya na jeshi la nchi jirani ya Kenya ili tuweze kuwabaini waharifu waliohusika na kuwafikisha mbele ya sheria” alisema Kamugisha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment