Na Dinna Maningo,Tarime
WAJUMBE wa Baraza la mamlaka Mji mdogo wa Tarime mkoani Mara wameiomba halimashauri ya wilaya ya Tarime kustisha tenda za wazabuni wanaoshindwa kutimiza mapato.
Hayo yamebainika katika kikao cha baraza la wajumbe wa mamlaka ya mji mdogo wa Tarime kuwa kuna mzabuni aliyechukuwa tenda stendi ya wilaya vikiwamo na vibanda na choo cha stendi lakini amekuwa halipi mapato na hivyo kuiingizia mamlaka hiyo hasara.
Wajumbe hao wameiomba Halimashauri kumsitishia tenda mzabuni Bw. Piter Keba Wangwe kwa madai kuwa amekuwa akikwepa kulipa ushuru kwa muda mlefu.
Mzabuni huyo anadaiwa kutolipa mapato ya choo kwa muda wa miaka 4 pia anadaiwa mapato ya vibanda vilivyopo stendi kwa muda wa miaka 3 nakuwa kiasi cha malipo ya vibanda kwa kila mwezi anatakiwa kulipa shilingi milioni moja na laki tano pamoja na kushindwa kulipa mapato ya hoteli yake iliyopo Stendi.
Mmoja kati ya wajumbe hao ambaye pia ni Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Mwita Mantago alisema mzabuni huyo anatakiwa kulipa mapato kila baada ya miezi 3 ambapo kwa mwezi mmoja malipo ni sh milioni 5 laki 7na 20 na amelipa malipo ya mwezi mmoja pekee na hivyo kuonekana kikwazo na ukwamishaji wa vyanzo vya mapato vya mamlaka ya mji.
Mantago aliomba Mzabuni huyo kuongezewa ushuru kwa madai kuwa hata ushuru wa stendi anao lipa malipo yake ni kidogo hayaendani na mapato halisi anayoyapata toka katika stendi hiyo ya magari kwani hamekuwa akitoza magari na maroli yaliyo nje ya stendi.
"Mkurugenzi wa Halimashauri tunakuomba umwondoe huyo mzabuni wapewe wazabuni wengine kwanini alipie ushuru wa stendi pekee na wakati anamiliki choo,hoteli na maduka!na hisitoshe anazaidi ya miaka 4 hajalipa ushuru wa choo na wakati kila mtu anapotaka kwenda kujisaidia chooni analipia sh. mia 200,ana muda wa miaka 3 hajawahi kulipia ushuru wa vibanda vilivypo stendi na nikwanini mzabuni huyu huyu mmoja amiliki Stendi,maduka na choo peke yake alafu anashindwa kulipa ushuru"alisema Mantago.
Wajumbe hao walisema kuwa ukuwaji wa vyanzo na kupanda kwa mapato ndani ya mamlaka ya mji yataongezeka endapo mzabuni huyo akiwajibishwa kulipa malipo yote anayodaiwa na vinginevyo asitishiwe tenda ili kuwakaribisha wengine wenye nia ya kuchangia maendeleo ya mji huo.
Hata hivyo mkurugenzi wa halimashauri ya Tarime Fidelis Lumato alimtetea mzabuni huyo na kudai kuwa amekuwa akilipa ushuru wa stendi kwa kiwango kinachotakiwa.
"Tunatakiwa kumpongeza huyu mzabuni kwa sababu anatulipa vizuri mapato, amelipa ushuru wa stendi kwa asilimia 56 amekuwa akivuka viwango cha mapato alichotakiwa na halimashauri.
Aidha wajumbe hao wameitaka halimashauri kutowaficha mikataba ya wazabuni kwa madai kuwa mamlaka hiyo ya mji haifahamu mikataba ya wazabuni na wala hata kiasi cha mapato kinachotolewa na wazabuni hao hakifahamiki na wala halmashauri imekuwa haiwafahaishi muda wa kukamilika kwa tenda za wazabuni.
Mkurugenzi Fideli alisema kuwa kwa sasa wamejipanga vizuri katika taratibu za kusaini mikataba ya wazabuni itakayo washirikisha wazabuni,wanasheria na Mkurugenzi wa mamlaka ya mji mdogo.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya John Henjewele alitaka baada ya kusainiwa kwa mikataba ya wazabuni itolewe copi na kisha ipelekwe katika mamlaka ya mji na sio kusalia halimashauri pekee.
Kwa hatua nyingine wajumbe hao wa mamlaka wameiomba halimashauri kuwashirikisha katika miradi kwa madai kuwa halimashauri hiyo imekuwa ikifanya miradi mamlaka ya miji bila hata kuwashirikisha wajumbe wa mamlaka hiyo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:
Post a Comment