Mwanza.
CHAMA cha Watu wenye Ulemavu wa ngozi-albino (TAS), Mkoa wa Mwanza,kimesema wanachama wake wameshindwa kuhudhuria kliniki ya tiba ya kansa na ngozi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Wilaya ya
Moshi mkoani Arusha, kutokana na kukosa fedha za nauli.
Kufuatia hali hiyo, chama hicho kimeiomba Serikali ya Rais JakayaKikwete kuisaidia jamii hiyo yenye ulemavu wa ngozi ili kuwawezesha kwenda kupata huduma hiyo muhimu kwa ajili ya kulinda uhai wa maisha
yao.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Mwanza na Katibu wa TAS Mkoa waMwanza, Bw. Mashaka Tuju wakati akisoma risala ya wanachama wa chamahicho, kwenye semina ya siku tano ya kujadili maendeleo ya watu hao wenye ulemavu wa ngozi katika Wilaya ya Ilemela jijini humo,iliyofanyika ukumbi wa kanisa la KKKT na kuhudhuriwa pia na mlezi waTAS Mkoani humo, Bw. Altaf Hiran Mansoor.
Kwa mujibu wa Katibu huyo wa TAS Mkoa wa Mwanza, mwaka jana 2011walitakiwa zaidi ya wanachama 12 wa chama hicho kuhudhuria kliniki ya tiba ya ngozi na kansa, na kwamba walishindwa kuhudhuria kwa sababu ya
kukosa nauli.
Hata hivyo, chama hicho cha albino, kimeuomba uongozi wa halmashauriya jiji la Mwanza kukisaidia jengo la ofisi ya kuendeshea shughuli zake, ikiwa ni pamoja na thamani za ofisi kwa ujumla.
Kuhusu uundwaji wa Katiba mpya, TAS Mkoa wa Mwanza kimemuomba Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha atakapounda Tume ya kukusanya maoni ya
uundwaji wa Katiba mpya aiagize kuwashirikisha walemavu hao kutoamaoni yao, bila ubaguzi wowote.
Awali, mwenyekiti wa Chama hicho cha albino Mkoa wa Mwanza, Bw. Alfred Kapole ameeleza kusikitishwa na mauaji yanayofanywa kwa baadhi ya walemavu hao wa ngozi, na kusema bado wanahofu kubwa juu ya usalama wa
maisha yao.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment