Thursday, September 9, 2010

SERIKALI KUONGEZA PATO NCHINI

SERIKALI ya Jamhuri Muungano wa Tanzania inatarajia kupanua uwezo wake wa ukusanyaji wa kodi ya ongezeko la Thamani VAT kuanzia sasa baada ya kuanza kutumika kwa mashine mpya za ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wafanyabiashara nchini kitu amcho imesemekana kitasaidia kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa leo mjini Musoma na Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoani Mara Bw Joseph Kalinga wakati akifungua mkutano wa kutambulisha mashine maalum ya ukusanyiji wa kodi na matumizi yake ambao umeshirikisha wafanyabiashara wa mkoa wa Mara.

Alisema kuanza kwa matumizi ya mashine hizo mpya za kukusanyia kodi pamoja mapato ya Serikali kutaongeza uwajibikaji na kutaondoa manung'uniko kutoka kwa wafanyabishara na TRA pamoja na kupunguza mianya ya ukwepaji wa kodi za Serikali kwa wafanyabiashara wasio kuwa waaminifu.

Akitoa maelezo kuhusiana na mabadiliko hayo mtoa mada katika mkutano huo Kabula mwemesi alisema kuwa mabadiliko hayo yatasaidia kuongeza pato la Taifa kwani mashine hizo zitakuwa na uwezo wa kuonyesha kila kitu ambacho kitakuwa kikifanywa.

Alisema kuna aina tatu ya mashine hizo ambazo ni Eletronic Tax Register,Electronic Fiscal Printer na Electronic Signature Device ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi sawa ingawa kwa watumiaji tofauti.
Aidha Kabula alisema kuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria mfanyabiashara kukwepa au kutaka chombo hicho kiende kinyume kwani hata kwa kufanya hivyo bado kumbukumbu zitaonyesha ulaghai katika kifaa hicho

Tayari Serikali imeteua kampuni sita nchini zitakazohusika kusambaza mashine hizo kwa wafanyabiashara nchi nzima kufutia mabadiliko ya sheria mpya ya kodi ambayo pia itamtaka kila mnunuzi wa bidhaa kuchukua stakabadhi kutoka kwa wauzaji.

Kwa mujibu wa Kabula makampuni hayo ni pamoja na Advatech Office Supplies Limited,Business MachineTanzania Limited,Pergamon Tanzania Tanzania Limited, Total Fiscal Solutions Limited,Checknocrats Limited na Compulynx Tanzania Limited

Aidha naye mmoja wa watoa mada katika mkutano huo Charles Stephen akijibu swali la mfanyabiashara mmoja kuwa ni nchi gani kusini mwa jangwa la sahara imefanikiwa katika utaratibu huo,mkufunzi huyo alisema utaratibu huo unatumiwa na nchi ya Kenya kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo umeonyesha mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa kodi ikiwa ni mara tatu ya kodi inayokusanywa hapa nchini.

Mbali na maswali kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali kwa wawezeshaji hao lakini baadhi walihoji je ni lini Serikali ilitoa zabuni katika kutafuta makampuni hayo kwani wanahofu isije ikawa ni biashara ya mtu.



No comments:

Post a Comment