Thursday, September 9, 2010

AHUKUMIWA MIAKA 30 NA VIOBOK 24 KWA WIZI WA SIMU

MUSOMA



MAHAKAMA ya wilaya ya Musoma mkoani Mara imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela na viboko 24 Makuyu Magayi mwenye umri wa maika 36 baada ya kukutwa na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi mkoani hapa Gabriel Bonanza alisema kuwa mnamo Decemba 22 mwaka jana mtuhumiwa alimvamia Peter Lenard maeneo ya Nyakato maziwa mjini hapa akiwa na silaha (kisu) na kumnyang’anya simu aina ya Nokia 6300 yenye thamai ya shilingi laki moja na nusu.


Akitoa hukumu hiyo hakimu Richard Maganga alisema kuwa hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo katika jamii.
Hakimu Maganga aliongeza kuwa mtuhumiwa atachapwa viboko 12 mbele ya hakimu wakati anaingia gerezani na viboko 12 wakati anatoka

Wakati huo huo habari zilizopo mjini hapa zinasema kuwa baadhi ya watu wamekamtwa na jeshi la Polisi mkoani hapa wakituhumiwa kuchana mabango ya wagombea sehemu mbalimbali zilipobandikwa.

Aidha mmoja wa wananchi ambaye alibahatika kuongea na Jambo Leo alisema kuwa kuna watui wanakuja wanabandika mabango hayo kwenye nyumba za watu pasipo makubaliano yoyote na hivyo kupelekea wahusika ambao hawataki kujihusisha na mambo ya uchaguzi kuyachana.

‘Unajua mtu anakuja anabandika bango kwenye nyumba ya mtu pasipo makubaliano na mwenye nyumba na wakati huo unakuta mwenye nyumba hataki kujihusisha na mambo ya uchaguzi jamani hapo tuseme ana makosa? Aliuliza mwananchi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Magati Alphonce.

Juhudi za kupata ufafanuzi kutoka kwa jeshi ala polisi hazikuzaa matunda kutokana Msemaji wa jeshi la Polisi mkoani hapa ambaye pia ni kamanda wa mkoa wa Mara Robert Boaz kuwa nje ya ofisi.

No comments:

Post a Comment