Thursday, September 9, 2010

CCM NA CHADEMA WAVUTANA MUSOMA

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Musoma mjini Bi. Haula Kachwamba amekanusha vikali tuhuma ambazo zilitolewa na viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani hapa kuwa baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kwa hupita mitaani na kuandikisha namba za kadi za kupigia kura na majina ya wahusika.

Akiongea kwa njia aya simu na gazeti hili Bi Kachwamba alisema kuwa ndio kwa mara ya kwanza anasikia taarifa hizo lakini ni za uzushi ila hao Chadema wasubiri oktoba 31 katika sanduku la kura


“Nashukuru sana kwanza taarifa hizo ndio nazisikia kwako kwa mara ya kwanza lakini naamini hakuna kitu kama hicho hao Chadema wao wasubiri oktoba 31 kwenye sanduku la kura”alisema katibu huyo.

Alisema kama kuna kitu kama hicho kinafanywa na viongozi wa CCM ni bora hao Viongozi wa Chadema wakaisaidia polisi ili wawakamate kwani ni kitu ambacho hakirugusiwi kwa mujibu wa sheria.

Katibu huyo alisema kuwa kwanza si rahisi kwa mtu yeyote kufanya hivyo kwani taarifa kwa tume ya uchaguzi hazitakuwa sahihi kama mtu yeyote atachukua kadi ya mtu ya kupigia kura ili ailete udanganyifu wa mtu kuitumia mara mbili kwa namba ile ile na picha ile ile.


‘Hao Chadema wao wasiogope na kuanza kuwalaghai wananchi kwani hicho kitu hakiwezekani katika kumbukumbu ya Tume ya taifa ya uchaguzi,yaani namba ile ile na picha ile ile si kweli hata kidogo.

Hivi karibuni mjini hapa mwenyekiti waChadema Musomsa mjini Bw Charles Kayele alisema kuwa mabarozi wa nyumba kumi ndio wanahusika kufanya mchezo huo huku wakitoa ahadi ya kuwapatia misaada wahusika wa kadi hiyo zilizotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi kwaajili ya kupigia kura.

Alisema zoezi hilo tayari limeendeshwa katika kata za Mwigobero,Kitaji,Kigera,Buhare,Mwisengena Mkendo kwa nyakati tofauti jambo ambalo linatia shaka kama uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki

Kayele alisema kuwa tayari viongozi wa chama hicho akiwemo mwenyekiti wa mtaa Rwamrimi (Chadema) Shaban Sondobhi wamewakamata viongozi hao wa CCM wakiendikisha majina na namba za kadi hizo za kura ambapo waliwafikisha taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.

Taarifa zinasema kuwa baada ya kuchukua namba na majina ya shahada hizo huzipeleka nchini Kenya kutengeneza kadi kama hizo ambazo zitatumika kupiga kura kwa watu wengine ambapo mpango huo inasemekana unaeleweka mpaka kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Katika hali ambayo mpaka sasa inaleta hali ya sintofahamu ,kamanda wa takukuru mkoa wa Mara alipopigia simu ili kuthibitisha madai hayo,alijibu kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo lakini anaweza kufanya hivyo endapo atapelekewa kwa maandishi

No comments:

Post a Comment