MTU mmoja mwanamke ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kukutwa umechomwa moto porini katika kijiji cha Nyambogo tarafa ya Girango katika wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya kamishina msaidizi Constantine Massawe,ameiambia Radio One Stereo kuwa mwili huo umeokotwa usiku wa Septemba 10 mwaka huu ambapo marehemu ametambulika kwa jina la Beldina Onyanga mwenye umri wa miaka 48.
Kamanda Massawe amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha kifo cha mwanamke huyo kinatokana na ugomvi wa mipanga ya ardhi aliokuwa akitumia kwa shughuli za kilimo.
Amesema hadi sasa polisi wa kituo kikuu cha kanda maalum ya Utegi wilayani Rorya inawashikilia watu wawili kwa mahojiano kuhusiana na kifo cha mtu huyo.
No comments:
Post a Comment