MUSOMA
CHAMA cha Wananchi CUF kimesema kuwa umaskini wa Watanzani umesababishwa na Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuendelea kutoa ahadi ambazo wanaelewa kamwe haziwezi kutekelezeka wakati nchi ni Tajiri.
Hayo yamesemwa na mgombea Makamu wa urais kupitia chama hicho Juma Duni Haji wakati akihutubia mamia ya Wananchi wa manispaa ya Musoma katika viwanja vya shule ya msingi Mkenddo mjini hapa,alisema kuwa kama chama hicho kimeshindwa kukamilisha ahadi zilizopita ambazo waliahidi mwaka 2005 iweje leo kila mkoa anahaidi tena ahadi za mamilioni.
Alisema kuwa tatizo la watanzania ni umaskini,ujinga ambao umeletwa na chama cha Mapinduzi CCM wakati wageni wanazidi kufaidi na baadhi ya viongozi ambao hawana moyo wa dhati katika kuwasaidia watanzania,aliongeza kuwa kama kweli chama hicho kinawajali watanzani ni watoto wangapi wa vigogo wanaosoma katika shule za kata kama sio mbinu za CCM kuweka wimbi kubwa la wajinga ili wawatale kwani maskini ni rahisi kutawaliwa.
‘Leo hii CCM wanasema wamejenga shule,hizo shule wamejengea nani asome wakati watoto wao hawasomi katika shule hizo? Ndugu zangu mie nawaambieni siku zote maskini na mjinga ni rahisi kutawaliwa kuliko tajiri na mwelevu huku taifa likiendelea kuwa la wanyonge” alisema Juma Duni Haji.
Mgombea huyo alisema kuwa kwa sasa watu wanaingia kwenye siasa kwa lengo la biashara lpamoja na kuwanyonya watanzania na si kuwatumikia,alisema sasa umefika wakati watanzania kufanya mabadiliko ambayo yataleta matumaini mapya kwa watanzania tofauti na ilivyo sasa.
Haji alisema kuwa kama chama chake kitafanikiwa kushika dola ya Tanzania watahakikisha elimu inakuwa bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu kwani nchi ina maliasili ya kutosha na hakuna sababu ya watanzani kuendelea kuwa wanyonge katika taifa lao,aliongeza kuwa mgombea urais wa chama hicho Profesa Ibrahimi Lipumba ni msomi ambaye anaelewa umuhimu wa elimu Hivyo kazi kwa watanzania ni kuondoa CCM katika madaraka.
‘Kama watanzania watatuamini na kutupatia madaraka katika nchi hii elimu itakuwa bure kwani nchi hii ni tajiri lakini bado wananchi wake wanakuwa wajinga kwa kukosa elimu iliyo bora,Lipumba ni msomi ambaye anaelewa umuhimu wa elimu kwa watanzania Hivyo nawaombeni mmpeni kura ili awe rais wa Tanzania”alisema Haji
Aidha katika mkutano huo mgombea ubunge kupitia chama hicho cha CUF Mstafa Juma Wandwi alisema kuwa katika nchi yoyote lazima wawepo wapambanaji ambao wamejitolea katika kuwatetea wanyonge.
Alisema yeye aliishaamua kufungwa kuwa maskini lakini watu wa Musoma wapate haki zao,aliongeza kuwa vijana wa jimbo la Musoma wasikubali kudanganyika kwani kwa kufanya Hivyo watakuwa wanajichimbia shimo la umaskini kwa miaka mitano pale watakapoichagua CCM kushika madaraka katika jimbo la Musoma.
Wandwi alisema kuwa mkoa wa Mara ulikuwa na viwanda vingi ambavyo vilisaidia kutoa ajira kwa vijana lakini leo viwanda Hivyo vimeuawa na serikali ya CCM,aliongeza kuwa Mwl Nyerere hakuwa mbinafsi na ndio maana aliweka viwanda kila mkoa ili viweze kutoa ajira kwa wananchi lakini baada ya zaidi za miaka 48 ya Uhuru leo ndio Kikwete anasema anataka kufufua viwanda huu ni ulaghai
Aidha akitoa mfano kwa wale wanaohoji kuwa yeye ni mzee Wandwi alisema kuwa uzee si hoja kwani hata Ibrahimu alipata mtoto akiwa na umri mkubwa,alisema yeye anakitu kichwani ambacho kitakuwa mwanga kwa wakazi wa jimbo la Musoma
“Eti leo kuna watu wanapita wanasema Wandwi mzee jamani mbona Ibrahimu alikaa muda mrefu bila mtoto lakini akapata akiwa mzee kwani ni kosa mimi kupata ubunge nikiwa mzee”? alihoji Wandwi
Mbali na mbunge huyo kujinadi kwa wananchi wa jimbo la Musoma pia madiwani wa kata kumi na tatu nao walipanda jukwaani kuomba kura kwa wananchi ili wapate ridhaa ya kuwakilisha chama hicho katika ngazi ya udiwani.
No comments:
Post a Comment