MUSOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma mjini mkoani Mara jana kimezindua kampeni zake mjini hapa uzinduzi ambao ulihudhuliwa na mamia ya wafuasi wa chama hicho katika uwanja wa shule ya msingi Mukendo huku baadhi ya makada wa chama hicho wakitofautiana kutoa takwimu za madarassa ambayo yamejengwa na mbunge anayetetea kiti hicho kwa miaka mitano ijayo.
Mgombea ubunge Musoma mjini Vedastus Mathayo
Mgombea ubunge Musoma mjini Vedastus Mathayo
Akishukuru wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo mgombea ubunge kupitia chama Mapinduzi (CCM) Vedastus Mathayo alisema kuwa yeye na chama chake kwa miaka mitano iliyopita wametekeleza mambo mengi ambayo waliahidi mwaka 2005,alisema kuwa wakati anaingia katika nafasi hiyo ya ubunge Musoma mjini kulikuwa na tatizo la elimu kutokana na ufinyu wa madarasa lakini kwa kipindi cha miaka 5 kila motto ameweza kwenda shule kwa upande wa secondary na msingi.
Mgombea huyo alisema kuwa mbali na kupambana na elimu lakini katika sekta ya afya hakuwa nyuma katika kuboresha majengo ya hospital ya mkoa huku katika zahanati kumi na moja zikijengwa katika kata kumi na tatu na zingine zikishindwa kujengwa kutokana na ukosefu wa kiwanja kama kata ya Mwigobero.
Mwantumu Mahiza naye alikuwepo
Mwantumu Mahiza naye alikuwepo
Alisema mwaka 2005 wakati anaingia madarakani hali ya hospital ya mkoa ilikuwa inatisha lakini kwa sasa anajivunia hospital hiyo kuwa katika kiwango kizuri ambacho kinastahili kutoa huduma kwa mwananchi hasa wakina mama wanapoenda kujifungua na hicho ni kitu kinachomsukuma kuomba tena ridhaa ya wananchi ili aweze kupambana katika kuijenga hospital ya Kwangwa ili iweze kutoa huduma kwa watu wa mkoa wa Mara na mikoa jirani na sio kukimbilia Bugando au KCMC n wengine Muhimbili.
‘Wakati naomba ridhaa yenu ile hospital ilikuwa katika hali mbaya lakini leo inapendeza na bado tutaenddelea kuirekebisha ili ipate hadhi ya kuwa hospital ya Rufaa” alisema Mathayo
Mbali na kuligusa suala la elimu Mathayo alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo kipaumbele chake kitakuwa elimu hasa katika upande wa madarasa,maktaba,maabara,nyumba za walimu na nyumba za askari polisi ambapo hata hivyo alisema tayari ujenzi umeanza kama alivyohaidi mwaka 2005.
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka 5 ijayo atahakikisha watoto hawakai chini kwani hilo atalifanya kwa kushirikiana na wazazi ili kupata madawati ambapo hata hivyo alisema kwa kiwango kikubwa madawati yapo katika shule za jimbo la Musoma mjini
Pamoja na kusema hivyo mgombea huyo alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita alihaidi kujengwa kwa kivuko na tayari ujenzi unaendelea na hivyo anamatumaini kukamilika kwa kivuko hicho kutaongeza fursa ya ajira kwa jimbo la Musoma mjini,aliongeza kuwa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi cha mjini Musoma nao utakamilika kwani kwa sasa tayari awamu ya kwanza imekamilika bado awamu ya pili nay a tatu ambayo ndiyo ya mwisho.
Mgombea huyo wa chama cha Mapinduzi katika nafasi ya ubunge jimbo la Musoma mjini alisema kwa upande wa ajira amefanikiwa kwani asilimia kubwa ya vijana wamejiajili katika kazi ya uendeshaji pikipiki (Bodaboda) na hivyo kupunguza wimbi la vijana wasiokuwa na ajira katika jimbo la Musoma na hivi karibuni aliwaletea sare ambazo imewasidia kupata mafunzo na kupewa namba kila mwendesha pikipiki.
‘Najivunia katika kipindi changu cha miaka mitano vijana wamepata ajira,kama mnavyoelewa kuliwa na tatizo la usafri hapa kwetu lakini nimelipigania sana bungeni na leo hii vijana wamepata ajira kwani kama nisingefanya Hivyo pengine kungekuwa na wimbi kubwa la vibaka hapa kwetu”alisema mgombea huyo
Mathayo alisema kuwa kama atapata nafasi hiyo tena ya kuwa mbunge katika jimbo la Musoma mjini kwa kipindi cha miaka mitano atahakikisha anapambana katika suala la viwanda vilivyoko ndani ya jimbo la Musoma huku akimuhimiza mwendeshaji wa kiwanda cha Mutex kuongeza uzalishaji ili wananchi wa Musoma wapate ajira,aliongeza kuwa pamoja na kupambana katika viwanda lakini pia atahakikisha viwanda vya samaki vinafufuliwa ikiwa ni pamoja na kujenga uwanja wa ndege katika eneo la Musoma vijini ambapo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo.
Pamoja na ahadi nyingi na kueleza utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa mwaka 2005-2010 na kuelezea ilani ya mwaka 2010-2015, Mathayo alisema kuwa wananchi wengi walishindwa kupata mapesa ya Kikwete kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu ya ujasiriamali Hivyo katika kipindi cha miaka mitano atajitahidi wananchi wa jimbo la Musoma wanapata elimu ya ujasiriamali.
Kuhusu na yeye kujiingiza katika biashara ambazo wananchi wa jimbo hilo wanafanya,Mathayo alisema kuwa kufanya kwake biashara imekuwa kama chuo kwani kumefanya kutokuwepo na mfumko wa bei katika jimbo la Musoma mjini kwani wafanyabishara wote wameamua kuuza kama kwa bei anayouza yeye.
Katika hali ambayo haikutegemewa mgombea huyo alishindwa kukanusha tuhuma dhidi yake ambazo zilipeleka baadhi ya sheli zake za mafuta kufungwa kutokana na kuchakachua mafuta,pia makada wa CCM kutoa twakimu ambazo zinakinzana mfano ni kada anayefahamika kwa jina la Musoma Bus ambaye alisema mbunge huyo amekuta jimbo la Musoma likiwa na shule nne za secondary lakini mpaka sasa kuna shule 14 huku mwenyekiti mstaafu wa CCM Musoma mjini Enock Ruyembe akisema kuwa wakati Matahyo aningia katika nafasi hiyo kulikuwa na shule tano za secondary na mpaka sasa kuna shule 15
Akikamilisha hotuba yake kwa wafuasi wa chama hicho kwa kuwatambulisha wagombea udiwani katika kata 13 za jimbo la Musoma mjini Mathayo alisema kuwa kuna watu wanazusha mambo na kama wanauhakika nayo wasimame jukwaani
‘Kuna mambo yanazunshwa lakini mimi sidhani kama ni vizuri kuzusha vitu ambavyo mtu havijui lakini kama mtu anavijua ni bora akasimama jukwaani akavisema na sio kuongea mitaani” alisema Mathayo
Katika kunogesha uzinduzi huo naibu waziri wa elimu na mafunzo Mwantum Mahiza aliyekuwepo katika uzinduzi huo alisema kuwa wananchi wasibabishwe wala kudanganywa kwa kuchagua vyama vya upinzani katika kwani kwa kufanya Hivyo maendeleo yaliyopo yatarudi nyuma.
Alisema kuwa kwa sasa Rais Kikwete anafahamika kimataifa Hivyo kumbadilisha na kuweka mtu mwingine kutafanya nchi hii kukosa maendeleo kwani Kikwete tayari anafahamika kimataifa kitu ambacho baadhi ya wananchi waliokuwa uwanjani hapo kupingana nacho.
No comments:
Post a Comment