Sunday, August 22, 2010

PINGAMIZI LATUPWA

Msimamizi wa uchaguzi kwa majimbo ya Bunda na Mwibara Cyprian Oyeir ametupilia mbali pingamizi la mgombea ubunge jimbo la Mwibara kwa tiketi ya Chadema dhidi ya mwenzake wa CCM  kufuatia ushahidi wa madai yake  kutojitosheleza kisheria.

Akiongea na waandishi wa habari jana mjini Bunda mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kusikilizamalalamiko hayo Oyeir amesema baada ya kusikiliza pande hizo mbili aliridhika na ushahidi uli0wasilishwa na upandewa utetezi na hivyo kuamua kuyatupilia mbali malalamiko ya ya mgombea huyo.

Kulingana na Oyeir jana (Ijumaa) mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Daudi Chiriko aliwasilisha madai kwake akimtuhumu mwenzake waCCM Alphaxard kangi Lugora kwamba alitoa rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni
zilizoendeshwa na chama chake wa kuwapata wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani.

Kwa mujibu wa msimamizi huyo katika malalamiko yake Chiriko alimwelezea Kangi kuwa alitoa rushwa ya mbegu za malando na mihogo pamoja na kupunguza nauli zamagari yake yanayofanya safari zakesehemu mbalimbali za jimbo hilo madai ambayo  amesema hayashughulikiwi na tume ya uchaguzi bali vyombo vya dola na kumtaka mgombea huyo ayawasilishe Takukuru ili yashughulikiwe.

Mbali na wagombea hao wengine wanaowania nafasi ya ubunge kwa jimbo hilo ni Mtamwega Toto Mugaywa wa TLP;Lawi Charles Magesa wa NCCRA-Mageuzi na Musita Vedastus Makaranga wa CUF.
                            
         Kwa msaada wa Christopher Maregesi Bunda

No comments:

Post a Comment