Sunday, July 5, 2015

Azam TV Yajipanga Kuwapatia Watanzania Matangazo Ya Kihistoria

Azam 6
Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando

Kituo cha Televisheni cha Azam ambacho kina umri wa chini ya miaka
miwili tu sasa kimejipanga kuwapatia Watanzania matangazo ya ubora wa
kiwango cha juu sana wakati wote wa kipindi cha msimu huu wa mchakato
wa uchaguzi mkuu wabunge na Urais mwaka huu wa 2015.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Azam TV Tabata jijini Dar es salaam leo Ijumaa 3 Julai 2015 Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando amesema
“Kwa kuwa tukio hili ni la kihistoria, Azam TV pia imedhamiria kutoa
matangazo ya kihistoria kwa ubora na ufanisi ukilinganisha na aina ya
matangazo ya televisheni ya matukio kama haya katika miaka ya nyuma.
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, vifaa bora pamoja na wafanyakazi
wenye ujuzi na weledi, Azam TV hasa kwa kutumia channel yake ya Azam
TWO, itatangaza matangazo ya uchaguzi wa mwaka huu kwa kipindi chote
cha Uchaguzi kwa kuanzia na harakati za hivi sasa za kutangaza nia kwa
wagombea mbalimbali hasa wale wa nafasi ya Urais kutoka chama tawala
cha CCM na baadaye kambi ya Upinzani.

Azam Televisheni imejipanga kutangaza mfulilizo wa Matangazo ya Moja
kwa moja kutoka Dodoma kwa kutumia vipindi vyake mbalimbali pamoja
na vipindi vingine maalum, pirikapirika zote, harakati zote pamoja na
matokeo yote ya kilele cha mpambano huo wa hatimae kupatikana kwa
mgombea huyo wa Urais wa CCM.
Azam 1
Azam 3 Kutoka kushoto Ni Meb fundi mitambo wa Azam TV, Taji Liundi Mtangazaji na mfanyakazi mwenzao

Tido Mhando amesema “Kuanzia Jumatano July 8 hadi Jumatatu July 13 kikosi cha wafanyikazi wa Azam Televisheni kitapiga kambi Dodoma kueleza kwa kinaga ubaga kila jambo litalokuwa linatokea huko na kwa undani sana ikitumia wachambuzi wenye ujuzi pamoja na kupata na kuzitoa habari za uhakika kwa haraka iwezekanavyo”.

“Matangazo haya yataanzia tangu mapema asubuhi kwenye kipindi chake
cha matangazo ya asubuhi kijulikanacho kama Morning Trumpet, kipindi
maalum cha saa moja wakati wa mchana kuanzia saa saba, kipindi cha
jioni cha Alasiri Lounge, taarifa ya habari maalum ya saa mbili kutoka saa
mbili kamili usiku pamoja na kipindi maalum cha usiku kuanzia saa nne na
nusu hadi saa sita usiku”.

Akiendelea kuongea mbele ya waandishi wa habari Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando Tido Mhando aliongeza kwa kusema “Wakati wa kilele cha hekeheka hizi za huko Dodoma yaani tarehe 11 July na 12 July ambapo mkutano mkuu wa CCM unafanyika, Azam Televisheni itakuwa na matangazo ya moja kwa wakati wote wa mkutano huo na baadae”.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huu, Azam Televisheni itatangaza pia
mikutano na mipango mingine kama hii kwa upande wa vyama vingine vya
kisiasa.
Azam 5
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando

Utaratibu wa matangazo haya ya uchaguzi utaendelea hivi hivi wakati wa
kipindi chote cha kampeni kuanzia mwezi wa August hadi tarehe yenyewe
ya uchaguzi hapo Octoba 25.

Labda ni wakati wa kipindi hicho cha uchaguzi kamili ambapo Azam
televisheni imejiimarisha zaidi kuweza kuwapatia watazamaji wake
matangazo bora ya kisasa zaidi kuliko wakati wowote katika historia ya
utangazaji nchini hapa.

Kwa kuzingatia umuhimu wa uchaguzi na upatikanaji wa habari za uhakika
kwa watanzania Azam imeweka dhamira hii kama sehemu ya historia kwa
kutimiza wajibu wa msingi wa vyombo vya habari kwa umma wa
watanzania.

Kwa kutumia studio bora kuliko zote karika kanda hii ya Afrika pamoja na
vifaa vingine vya kileo kabisa, Azam televisheni itatangaza mfulilizo na
moja kwa moja matukio yote muhimu ya wakati huo wa kupiga kura,
kuhesabiwa kwa kura na hatimae kutangazwa washindi wa nafasi ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge wa bunge la
Muungano na Baraza la wawakilishi, Zanzibar.

Kujiamini huku kwa Azam Televisheni katika kutekeleza lengo hili kubwa
kunafuatia kuajiriwa kwa kundi la watangazaji mahiri ambao kwayo ujuzi na
uelewa wao pamoja na misingi ya weledi itakayozingatiwa bila ya shaka
utawezesha ari hii kutekelezwa kwa kiwango cha mafanikio makubwa.
Miongoni mwa watangazaji hao ni Charles Hilary, Ivona Kamuntu, Fatuma
Nyangassa, Baruani Muhuza, Hassan Mhelela, Faraja John, Raymond
Nyamwihula, Jane Shirima, Phillip Cyprian, Mwanga Kirahi, na Taji Liundi.
4
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mtendaji Mkuu Uhai Productions/Azam TV Dunstan Tido Mhando

Tuna amini ya kwamba kundi la watangazaji hawa wenye ujuzi na wengine
wachache ambao watakuja hivi karibuni wakiungana na wale vijana
wasomi ambao tayari wamekuwepo wataweza kufanikisha ile ari ya
kukifanya kituo cha Azam Televisheni kuwa bora zaidi katika kanda hii.
Mbali na kuimarishwa kwa kitengo cha habari lakini mipangp na mikakati
bora imeandaliwa ya kupata vipindi vingine bora vya aina mbalimbali
ambavyo vitatayarishwa kwa kiwango cha juu na cha hadhi ya kimataifa
ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa matangazo ya
vipindi vya michezo na matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu
ikiwa ni pamoja na yale ya ya ligi kuu ya kandanda Tanzania yaani
Vodacom Premier League.

Kwa kuwapatia watazamaji wetu na watanzania kwa ujumla matangazo
haya bora ya vipindi vizuri vya televisheni, tunauhakika wanunuzi wa
ving’amuzi vya Azam watakuwa wanapata wakitakacho na zaidi.

No comments:

Post a Comment