Monday, July 27, 2015

Muuza Dagaa ashinda ubunge viti Maalum Mara

MCHUUZI wa dagaa kwenye mwalo wa Mwigobero uliopo Manispaa ya Musoma,Agnes Methew,ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kutafuta Mbunge wa viti maalumu(CCM) mkoa wa Mara.

Akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi huo,Samwer Kiboye ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya,alisema wajumbe wameonyesha namna ambavyo hata mtu wa chini anaweza kushinda tofauti na inavyozungumzwa.

Alisema wao watu ambao wamekuwa wakizungumza pembeni ukiwa Chma cha Mapinduzi huwezi kupata nafasi ya uongozi kama hauna fedha jambo ambalo sio kweli kwa kuwa yeye amechaguliwa bila kujali kipato chake na kuwashinda walioonekana na kipato cha juu na majina makubwa.

“Niwashukuru sana wajumbe kwa kunipigia kura za kishindo na kunifanya niibuke mshindi kati ya wagombea wengine 9 wanachma wenzangu ambao nilikuwa nikishindana nao ndani ya uchaguzi huu.

“2010 nilikuja kwa mara ya kwanza kuwaomba nafasi hii lakini kura hazikutosha lakini safari hii mmeamua kunichagua mimi muuza dagaa na kuudhilihisha umma ndani ya CCM hata mtu wa hali ya chini anaweza kupewa uongozi.

Kwa jinsi mlivyoniamini naomba   niwahakikishie sito waangusha na kikubwa naomba tupeane ushirikiano na pale nitakapofanikiwa kuingia bungeni nitakuwa mstari wa mbele kuzungumzia masula yanayowahusu wanawake katika kufanikisha chachu ya maendeleo,”alisema Agnes.

Wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa,mgombea huyo aliwatoa chozi wajumbe baada ya kuomba kura huku akilia akiomba kuchaguliwa muuza dagaa kwa kwa kipindi chote amekuwa yupo na wajumbe katika kiangazi na mvua.

Katika uchaguzi huo,Agnes Methew alichaguliwa kwa kupata kura 418 kati ya kura 641 zilizopigwa na kufuatiwa na Chrstina Samo aliyepata kura 226 huku Mwenyekiti wa (UWT) mkoa wa Mara,Nancy Msafiri akipata kura 208 na kushika nafasi ya tatu.

Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo,msimamizi wa uchaguzi,Samwer Kiboye,aliwahasa wagombea wote kukubalina na matokeo kwa kuwa uchaguzi ni wa haki ili kuweza kushirikiana kwa pamoja kutafuta kura za CCM katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba.
 
No comments:

Post a Comment